Habari za Punde

Wananchi wa Makondeko Wakabidhiwa Mradi wa Kisima cha Maji Baada ya Kukamilika Kuondoa Tatizo la Maji.

Na.Takdir Suweid. Maelezo Zanzibar.
Uongozi wa Jimbo Pangawe umejipanga kuwatatulia Wananchi Tatizo la Maji kwa kushirikiana na Wafadhili.
Hayo yameelezwa na Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Thuwaiba Jenu Pandu wakati akikabidhi kisima na Tanki la Maji kwa Wakaazi wa Mtaa wa Makondeko,kisima ambacho kimechimbwa na Diwani huyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rafiki Elimu society.
Amesema katika Jimbo la Pangawe kwa kushirikia na taasisi hiyo na Afrika Muslim wameshachimba zaidi Visima 30 maeneo mbalimbali ili kutatua tatizo la Maji.
Hivyo ni vyema Wananchi kuwaunga mkono kwa kuienzi na kuitunza Miondombinu ya Maji ili iweze kuwa endelevu na kuondosha kero kwa Wananchi.
Aidha amewakumbusha Madiwani wenzake kutafuta ufadhili wa kutatua Matatizo mbali mbali yanayowakabili Wananchi wao na sio kuwaachia Viongozi wa Majimbo na Serikali pekee.
Hata hivyo ameahidi kushirikiana na Viongozi wa Majimbo katika Wilaya hiyo katika kuzitafutia ufumbuzi kero za Wananchi ili wazidi kujenga imani na Viongozi wao na kukifanya Chama cha Mapinduzi kuendelea kushika Dola.
Kwa upande wake Mwangalizi wa Kisima hicho Fatma Shilingi amesema kwa muda mrefu wanasumbuka kwa kuifuata huduma hiyo masafa ya mbali lakini kuchimbwa Kisima hicho kutaondosha usumbufu wanaupata Wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.