Habari za Punde

NAIBU WAZIRI NYONGO AONGOZA KIKAO CHA MARIDHIANO NA KUPOKEA OMBI LA MWEKEZAJI



NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nzega ili kusikiliza maombi na kutatua  changamoto za wachimbaji wadogo wa madini Aprili 27 mwaka huu
NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kulia akihoji jambo kwa wachimbaji waliokuwa wakilalamika kutopewa leseni kwenye eneo ambalo waliliomba jambo ambalo RMO alipaswa kukaa na pande hizo kutafuta muafaka
NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na waandishi wa habari juu ya makubaliano yaliyofikiwa mara baada ya wajumbe kujadili maombi ya mwekezaji ya kutaka kupunguziwa gharama ya ununuzi wa madini ya dhahabu baada ya uchenjuaji wa marudio wa mchanga wa dhahabu ulioachwa na mwekezaji mkubwa wa madini wa kampuni ya  Resolute iliyokuwa ikifanya shughuli zake wilaya ya Nzega kufunga mgodi
NAIBU waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Nzega kulia Godfrey Nyapula wakati wa kikao na wachimbaji wadogo wa madini kilichofanyika kwenye ofisi za Mkuu huyo wa wilaya Aprili 27 mwaka huu
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini Proffesa Shukrani Manyaa akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua zinazofuata baada ya kikao cha kuridhia ombi la mekezaji ili utekelezaji wake uwekwe katika utaratibu unaokubalika kisheria
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, akiongoza kikao kilichohudhuriwa na Katibu Mtendaji wa TumeyaMadini, Prof. ShukraniManya, MkuuwaWilayayaNzega, Godfrey Ngupula, Afisa  Madini Mkazi wa Mkoa waTabora, Mhandisi Mayingi Makalobela, Mkuu wa Chuo cha Nzega, Nuru Shaban Kamati ya Ulinzi na Usalama  wilaya ya Nzega pamoja na mwekezaji wa uchenjuaji wa marudio, RashedShabout Said.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa waTabora, Mhandisi Mayingi Makalobela akitoa maoni yake juu ya ombi la mwekezaji Rashed Shabout Said wa uchenjuaji wamarudio ya mchanga ulioachwa na kampuni ya resolute baada ya mgodi huo kufungwa.

SERIKALI  imeridhia ombi la kupunguza gharama ya ununuzi wa dhahabu unaofanywa na mwekezaji Rashed Shabout Said wa kampuni ya Ashery Construction &Matinje gold Extraction yauchenjuaji wa marudio ya mchanga wa dhahabu ulioachwanakampuniya Resolute iliyofunga shughuli zake za uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu mwaka 2014.

Makubaliano hayo yalifikiwa Aprili 27, 2020 wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus  Nyongo kilicholenga kujadili ombi la mwekezaji Rashed Shabout Said anayechenjua dhahabu kwenye mabaki hayo ya mchanga wa dhahabu ulioachwa na kampuni ya Resolute iliyokuwa ikichimba dhahabu wilayani Nzega,MkoaniTabora.

Pamoja na NaibuWaziri Nyongo kikao hicho kiliwahusisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini,Profesa Shukrani Manya, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora Mayingi Makalobela, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula, Mkuuwa Chuo cha Madini kampasi yaNzega, Nuru Shabani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nzega pamoja na  ujumbe ulioambatana na mwekezaji huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Naibu Waziri Nyongo alisema, kikao kimeridhia ombi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa na mwekezaji ikiwa ni kushusha bei ya kumwuzia dhahabu kiasi kilichopunguzwa kimsaidie kulipia  gharama nyingine anazozitumia katika uwekezaji huo.

Nyongo alisema Rashed aliomba kupunguzi wa gharama ya dhahabu anayoinunua serikalini mara baada ya uchenjuaji, kuondolewa gharama za watumishi wanaoshiriki katika kusimamia mchakato mzima wa uchenjuaji wa mchanga huo pamoja na kuondolewa malipo ya mrabaha nakurudishiwa pesa zilizolipwa kama mrabaha kwa awali mbili za uchenjuaji zilizopita.

Nyongo alibainisha kuwa Wizara kwa kushirikiana na Tume ya madini zimeridhia kupunguza gharama ya kuuza dhahabu kwa  mwekezaji huyo na kwamba huduma nyingine na malipo ya mrabaha yatapaswa kulipwa kama kawaida  kwa mujibu wa sheria.


Kwaupande wake, KatibuMtendajiwaTumeyaMadini, Prof. Shukrani Manya alisema ombi la mwekezaji limepokelewa na kwamba hatua inayofuata nikwenda kupitia na kurekebisha mkataba ikiwani pamoja na kupeleka maoni yaliyofikiwa na kikao hicho kwa mamlaka nyingine ili kumwezesha mwekezaji huyo kufanya kazi yake kwa tija na bila manung’uniko.

Akizungumza na waandishi wa habari mwekezaji Rashed, aliishukuru serikali kwa kupokea na kufanyia kaziombi lake na kukiri hakutegemea kuwa angesaidiwa kw aharaka namna ilivyofanyika nakukiri kwamba hakika Serikali ya Awamu ya Tano inasikilizana kutatua changamoto za wananchi.

“Nashukuru sana kwa serikali hadi Naibu Waziri kuja kunisikiliza kwa kweli Wizara ya madini nisikivu sana, nashukuru sana” Rashed alikazia.

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona Rashed alisema kumekuwa na changamoto ya usafirishaji wa madini kutokana na ndege nyingi za nje kusitisha safari zanje hivyo inakuwa ngumu kwa kuendesha biashara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.