Habari za Punde

SEKTA YA UTALII NCHINI INAPITIA KIPINDI KIGUMU SANA" NAIBU WAZIRI MHE.CONSTANTINE KANYASU

Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto akisalimiana na Abel Chang'a kwa kugonga miguu ikiwa ni salamu inayoshauriwa kutumiwa kwa sasa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ili kuepuka kuambukizana virusi vya ugonjwa huo mara baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kumaliza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Irindi kilichopo katika wilya ya Kilolo mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa  Kijiji cha Mahenge mara baada ya kufanya ziara ya kuwasikiliza na kujionea athari zilizosababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu walivyoharibu mazao katika mashamba ya Wananchi hao katika mkutano uliofanyika katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Lugalo iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kufuatia kuvamiwa na makundi ya Simba ambayo yalikula ng'ombe wawili wa mkazi wa Kata hiyo Bw.Aloyce Nziku ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi watoe taarifa mapema  wanapovamiwa na Wanyamapori.
Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto akisalimiana na Mchungaji kwa kugonga miguu ikiwa ni salamu inayoshauriwa kutumiwa kwa sasa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ili kuepuka kuambukizana virusi vya ugonjwa huo mara baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kumaliza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Irindi kilichopo katika wilya ya Kilolo mkoani Iringa
Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto akisalimiana na Abel Chang'a kwa kugonga miguu ikiwa ni salamu inayoshauriwa kutumiwa kwa sasa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ili kuepuka kuambukizana virusi vya ugonjwa huo mara baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kumaliza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Irindi kilichopo katika wilya ya Kilolo mkoani Iringa

 
Na.lusungu helela
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema sekta ya Utalii nchini  inapitia katika kipindi kigumu sana tangu nchi ipate Uhuru.

Amesema kutokana na  mlipuko wa virusi vya Corona  kuanzia mwezi Februari mwaka huu idadi ya watalii  wanaotembelea vivutio vya Utalii nchini imezidi kupungua hadi kufikia hakuna Mtalii kabisa.


Ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Irindi, Ikula, Lugalo na Mahenge katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa  wakati  alipofanya ziara  ya kikazi ya Siku moja ya  kutembelea kujionea uharibifu wa mazao uliofanywa na wanyama wakali na waharibifu katika mashamba ya wanavijiji hao.


Mhe.Kanyasu amesema tangu ugonjwa huo  kuanza  Sekta hiyo ambayo kwa zaidi asilimia 95 hutegemea watalii wa kutoka nje za nchi kuja kutembelea vivutio vya utalii imeathirika sana kimapato.

Akizitaja Taasisi za Uhifadhi nchini zilizoathirika na mlipuko wa virusi vya Corona ikiwemo Shirika la Hifadhi Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi Ngorogoro, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania pamoja Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Amesema watalii wengi kutoka Nchi za nje baada ya kutokea ugojwa huo watalii wengi waliokuwa wamepanga kuja nchini waliahirisha safari zao huku wengine walizifuta kabisa.

Hata hivyo, Mhe.Kanyasu ametoa wito kwa watalii waliokuwa wamepanga kutembelea vivutio vya utalii nchini wasizifute safari zao badala yake waziahirishe ili baada ya ugonjwa huu kuisha waweze kuja.

Akizungumzia athari za utalii nchini Tanzania, Mhe.Kanyasu amesema ugonjwa huo umesababisha hoteli za kitalii zilizopo katika Hifadhi zote nchini kufungwa kwa vile hakuna watalii wanaokwenda kutalii

Aidha, Amesema hoteli kubwa zilizo katika miji kavile Dar es Salaam, Kilimanjaro pamoja na Arusha zimefungwa kwa kukosa watalii.

Amesema kuibuka kwa ugonjwa huo kumpelekea Mashirika ya ndege Duniani kusitisha kutoa huduma za usafiri kwa hofu ya kusambaza zaidi ugonjwa huo kwa idadi kubwa ya watu hivyo sekta ya utalii imezidi kusinyaa siku hadi siku

Mbali na athari hizo, Mhe.Kanyasu amesema kusinyaa kwa sekta ya utalii ambayo imekuwa ikichangia asilimia 17 ya pato la Taifa imepelekea idadi kubwa ya watu kukosa ajira.


Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi wote kuchukua tahadhari juu ya virusi vya Corona kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu ipasavyo

Aamewataka kuhakikisha hawapeani salamu kwa kushikana mikono pamoja na kuhakikisha wananawa mikono pale inapohitajika.

Kwa upande wake Mbunge wa Kilolo, Mhe.Venance Mwamoto amewataka wananchi walioharibiwa mazao yao na wanyama wakali na waharibifu wawe watalivu Serikali inayafanyia kazi maombi yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.