Habari za Punde

Mwakilishi ataka watoto wasiuziwe barakoa

Na Takdir Suweid, Mkoa wa Mjini Magharibi

Viongozi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Mjini wameombwa kusimamia maagizo yaliotolewa na Serikali ya kuondosha mikusanyiko isiokuwa ya lazima katika maeneo mbalimbali yakutoa huduma ili kunusuru kuongezeka Janga la Corona. 

Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa viti maalum Sada Ramadhani Mwendwa wakati alipokuwa akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari,huko Amani Wilaya ya Mjini. Amesema kuna mikusanyiko ya Watu katika maeneo ya Darajani,Saateni na Soko jipya la Kariakoo jambo ambalo linaweza kusababisha kuongezeka maambukizi ya Virusi vya Corona. 

Aidha amesema Baraza hilo limeongeza idadi ya masoko ili kuondosha mikusanyiko isiokuwa ya lazima lakini baadhi ya Watu wanakaidi na kuhatarisha maisha yao. 

Hata hivyo ameliomba Baraza hilo kusimamia kwa kuhakikisha Watoto hawauzi Vibarakoa ili kuwalinda na Virusi vya Maradhi ya covid 19 .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.