Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni akabidhi Barakoa kwa Wananchi jimboni kwake

Na Takdir Suweid

Uongozi wa Jimbo la Magomeni umesema utaendelea kuunga Mkono Serikali kwa kutoa Misaada mbalimbali kwa Wananchi wao ili kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwalinda Wananchi na Maradhi.
Akikabidhi vibarakoa zaidi ya elfu sita,vyenye Thamani ya sh.milioni 5,laki 4 na 40 huko Tawi la Ccm Magomeni Mwakilishi wa Jimbo hilo Rashid Makame Shamsi amesema wameamua kukabidhi Vibarakoa hivyo ili Wananchi wao waweze kujikinga na homa kali ya mapafu ya Covid 19.
Aidha amewaagiza Mabalozi wa Nyumba 10 katika Jimbo hilo kuwapa kipao mbele Wananchi wa kipato cha chini ili waweze kushiriki katika sehemu muhimu za kutoa huduma kama vile Hospitali na Masokoni.
Hata hivyo amewataka Wananchi hao kuacha kuazimana Vibarakoa ili kuepukana na kuambukizana Maradhi katika familia.
Kwa uapnde wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Magomeni Mahmoud Juma Ali amewataka Wananchi kuacha dharau na kufuata maelekezo wanayotolewa na Wataalamu wa Afya katika kukabiliana na Virusi vya Corona.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.