Habari za Punde

Balozi Ali Karume Ajitokeza Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM


Balozi Ali Abeid Amani Karume akionesha Mkoba wake uliokuwa na Fomu za Kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo, alipofika leo akiwa Mwanachama wa Pili kuchukua Fomu za kuwania kupata nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi mwaka 2020. Hafla hiyo imefanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.leo 15/6/2020
Balozi Ali Abeid Amani Karume Mwanachama wa Pili wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar  kujitokeaza kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar akiwa na wapambe wake kwa ajili ya uchukuaji wa Fomu leo. 
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akipokea fedha kwa ajili ya malipo ya uchukuaji wa Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kutoka kwa Mhe Balozi Ali Karume , akiwa manachama wa Pili wa CCM kujitokea leo kuchukua fomu za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.hafla hiyo imefanyika katrika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Mhe. Ali Abeid Karume, hafla hiyo imefanyiuka leo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 
Mgombea nafasi ya Urais kupitia CCM Mhe. Baloziu Ali Karume akisoma Fomu yake ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Katibu wa Idara ya Oganizeshani ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi Fomu ya Kugombea Urais Mwanachama wa CCM Mhe. Balozi Ali Karume, alipofika leo kuchukua fomu  kwa ajili ya kupata ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mwaka  Oktoba 2020. Hafla hiyo imefanyika katiuka Afisi ya CCM Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.