Habari za Punde

MKURUGENZI KAGURUMJULI AWEKA HISTORIA KINONDONI KUKAMILISHA MIRADI YA BILIONI 231.8 KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ALAT YA MTUKUNU TUZO

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT), Bwana Elirehemu Kaaya akimkabizi cheti cha shukrani Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kutokana na umahiri wa utendaji kazi wake.
Msthiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita akimkabidhi tuzo ya umahiri Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndug. Aron Kagurumjuli kutokana na utendaji kazi wake na kuleta maendeleo makubwa katika Halmashauri hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita katikati, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, Mkurugenzi Aron Kagurumjuli wakiwa kwenye kikao cha kuvunja baraza la madiwani la Halmashauri hiyo.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limeweka historia ya ukamilishaji wa miradi mikubwa kwa kipidi cha miaka mitano ya uongozi wa Mhe. Rais Dk. John Magufuli iliyogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 231.8.

 Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri hiyo katika kipindi hicho Mkurugenzi Ndug. Aron Kagurumjuli amesema kuwa kwaupande wa miradi ya kisekta imefanikiwa kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na miradi ya Maendeleo kwa Wananchi.

Kagurumjuli amesema kuwa miradi hiyo inajumlisha ujenzi na ukarabati wa Vyumba vya Madasara, Vyoo kwa shule za msingi na Sekondari, ununuzi wa madawati kwa shule hizo, ujenzi, ukarabati na upanuzi wa Zahanati , Vituo vya Afya na Hospitali, ujenzi wa miradi ya Masoko na uwekezaji.

Ametaja maeneo mengine kuwa ni miradi ya barabara kwa kiwango cha  lami km. 189 kutoka km. 134, kupitia mradi wa DMDP, TARURA, uendelezaji  wa miradi ya kilimo na mifugo, ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuzalisha mbolea mboji, hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na utoaji wa asilimia 10 ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu.

Aidha amefafanua kuwa Halmashauri katika kipindi cha miaka mitano hadi kufikia Juni mwaka huu imetumia kiasi cha shilingi Bil. 3.3 kwa ajili ya kugharamia Elimu ya Msingi bila malipo, Bil. 2.2 Elimu ya Sekondari na hivyo kumpongeza Rais Magufuli kwa kuleta mpango huo.

Mbali na fedha hizo, lakini pia Manispaa imefanikiwa kujenga shule Nne za Msingi, ujenzi wa vyumba vya madarasa kutoka 983 Oktoba 2015 hadi kufikia 1147, ukarabati wa vyumba  111, matundu ya choo kutoka 686 hadi 1167, ununuzi wa Madawati kutoka 12,962 hadi kufikia 28,705, Maktaba kutoka 13 hadi 22, majengo ya utawala sita pamoja na ofisi za walimu kutoka 49 hadi  49.

Kwaupande wa shule za Sekondari Manispaa imefanikiwa “kujenga vyumba vya madarasa 48, katika shule mpya za Mzimuni, Kijitonyama, Magomeni, Mbezi juu, Mivumoni, Shule mpya mbili za Alevel, ukarabati wa vyumba 21, Matundu ya choo kutoka 389 hadi 473, Viti na Meza kutoka 19,353 hadi 25,067, Hosteli moja, Nyumba Nne  Walimu maabara kutoka 63 hadi 120,  majengo ya utawala saba” ameeleza Kagurumjuli.

“ Kwaupande wa Afya tumefanikiwa kujenga Zahanati Nne, vituo vya Afya vitatu ambapo kimoja ni kituo cha Afya Kigogo chenye Ghorofa tano, Hospitali mbili za Ghorofa, upanuzi na ukarabati wa Zahanati sita, Magari ya kubebea wagonjwa matatu, Nyumba za watumishi mbili, Wodi ya Baba, Mama na Mtoto (RCH) 14” ameeleza Kagurumjuli.

Kwaupande wa Masoko, amesema “ tumekuwa na miradi ya kimkakati na uwekezaji ambayo ni Soko la kisasa la Magomeni, Tandale, vituo vya ukusanyaji wa mapato sita, uwanja wa mpira Mwenge pamoja na Stendi ya daladala ya Mwenge” ameongeza Kagurumjuli.

Kwaupande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala na Serikali za Mitaa (ALAT), Bwana Elirehemu Kaaya akitoa salamu  ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanya kazi nzuri na kusema kuwa ndio Halmashauri pekee Tanzania iliyoweka historia ya utekelezaji wa miradi yake kwa wakati.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo pia imeweka historia ya kuwa na Mkurugenzi mchapa kazi, mwadilifu,msikivu, namwenyekusimamia maendeleo na hivyo kumtukunu cheti cha shukrani ikiwa ni katika juhudi za kutambua mchango wake.

Awali akitoa salamu za shukrani, Mstahiki Meya Mhe. Benjamini Sita amesema kuwa Halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi Kagurumjuli imeweka historia Tanzania nzima kwani imefanya mambo makubwa katika kipindi cha uongozi wao na hivyo kumtunuku tuzo ya kutambua mchango wake.

Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine wanaondoka wakiwa wameacha alama kubwa ambayo imeweka historia na kusema kuwa iwapo watakuwa na nafasi nyingine ya kurudi watafanya mambo makubwa mengine kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Kinondoni.

“Mkurugenzi hongera sana, umefanya mambo makubwa, kwenye uongozi huu tumeshirikiana kama timu, hukujali itikadi za vyama, umewavumilia madiwani wangu, mwisho wa siku umefanya jambo ambalo historia yake tunaiandika leo hii” amesema Mhe. Sita.

Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusino Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.