Habari za Punde

“Wizara ya Katiba na Sheria na Tume ya Haki za Binadamu zina Wajibu wa kulinda haki za wananchi”-Jaji Mstaafu Mwaimu


Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibari, Mhe.Khamis Juma Mwalim akipokea Mpango mkakati wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alipomtembelea Ofisini Kwake Mjini Unguja Zanzibar. 

Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Mhe.Khamis Juma Mwalim na Mgeni wake Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakiendesha kikao kifupi kuhusu haki za binadamu ambapo ujumbe watu wa haki za binadamu ulimtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (wa pili kulia) akizungumza katika kikao kifupi kuhusu haki za binadamu alipomtembelea Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibari, Mhe.Khamis Juma Mwalim (wa tatu kulia) katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mjini Unguja Zanzibari, wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo,  Mohamedi Khamis Hamadi (wa kwanza kulia), pamoja na watumishi kutoka Ofisi ya Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibari.

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO                                                                                               
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utwala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu leo Juni 4 amekutana na Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mappinduzi ya Zanzibari, Mhe.Khamis Juma Mwalim na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya haki za binadamu.

Katika Mkutano huo uliwakutanisha wajumbe kutoka tume hiyo pamoja na Ofisi ya Katiba na Sheria Zanzibari, Jaji Mwaimu alieleza namna Tume hiyo inavyoendeleza uhusiano kati yake na Wizara ya Katiba na Sheria katika kutekeleza majuku ya kulinda na kutimiza wajibu wa kuwapatia wananchi haki yao pale inapokuwa imeingiwa na dosari.

“Tumekuja kukutana na Mhe. Waziri lengo hasa ni kuendeleza uhusiano baina yetu na Ofisi yake, ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa kila mwananchi, lakini pia leo tumemkabidhi mpango mkakati wa tume wa miaka mitano kuanzia mwaka 2018/2023, nini hasa tutatekeleza katika kuweka usawa wa haki za binadamu na utawala bora hasa kwa watoto na wanawake”, Jaji Mstaafu Mwaimu.

Jaji Mwaimu alisema lengo la kukabidhi mpango huo ni kuwezesha Wizara na Serikali kujua uwazi wa tume hiyo katika utekelezaji wa majuku yake katika kulinda na kutoa haki kwa kila mtanzania kwenye maeneo ya haki za binadamu na utawala bora.

Aidha alisema kuwa ushirikiano kati ya Tume na Wizara ya Katiba na Sheria ni kitu muhimu na kwasababu wizara hiyo ina dhamana kubwa ya kulinda haki zikiwemo haki za binadamu, kwa hiyo ziara  ya kumtembelea Mhe. Waziri ni ishara ya kudumisha na kulinda utekelezaji wa haki kwa wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Mhe.Khamis Juma Mwalim alisema kuwa Wizara hiyo imekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wananchi ambao hawana uelewa wa sheria katika maeneo mbalimbali kupitia Taasisi zake ili kuwezesha upataikanaji wa haki kwa wananchi wa Zanzibari.

“Wizara ya Katiba na Sheria hapa Zanzibari imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya sheria katika mashamba mbalimbali,  miji na maeneo mengi ya mji wetu, lakini vile vile tumekuwa tukienda Pemba, na Mikoa mbalimbali, kwani  Idara ya Msaada wa sheria hasa pale Mhe. Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohahed Shien, alipomteua Mkurugenzi wa Idara kwa sasa  imekuwa ikienda mbio kwenda kutoa msaada kwa wananchi maeneo mengi ya Zanzibari”. Waziri Mwalim.

Alisema kuwa Sheria zipo nyingi kwa hiyo idara ya msaada wa Sheria imekuwa na wajibu mkubwa wa kuwapa wananchi nini wafanye wakihitaji kupata haki yao katika maeneo yao hasa maeneo yaliyoko vijijini kwani kuna unyanyasaji wa kinjia kwa  wanawake na watoto  kwa hiyo msaada wa sheria ni muhimu kwa wananchi wote.

Akizungumzia ripoti ambazo zilitolewa na tume ya  haki za binadamu, Waziri Mwalim alisema kuwa tume hiyo imejitahidi katika kutekeleza jukumu kubwa la kutoa ripoti ambazo miaka kadhaa zilisimama kutolewa kutokana na tume kutokuwa na Makamishna  na alitoa pongezi kwa Tume kufanya hivyo kwani Wizara inatakuwa na uwanda mpana wa kutoa maoni kabla ya ripoti hizo kupelekwa kwenye vyombo vya kutunga sheria likiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ni mawazo mazuri kutuletea ripoti hizi na mpango mkakati ili zituwezeshe kutoa maoni na kuleta huduma  zilizobora kwa wananchi wetu kwa kuzingatia haki za binadamu, naamini Mhe. Rais Magufuli aliwateueni kuwakilisha na kulinda haki za binadamu nje na ndani ya Nchi, endeleeni na jukumu hilo ambalo ni kubwa kwa nchi yetu” Alisem Waziri Mwalim.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.