Habari za Punde

JNIA WAPATIWA MAFUNZO YA UTAYARI WA KUPOKEA WATALII

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utayari wa kupokea watalii watumishi wa taasisi zinazotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati huu wa janga la Corona leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regina Hess akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utayari wa kupokea watalii watumishi wa taasisi zinazotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati huu wa janga la Corona leo jijini Dar es salaam. Ujerumani imekua ikiunga mkono juhudi za Serikali kwa kufadhili mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.
Baadhi ya washiriki wa  mafunzo ya  utayari wa kupokea watalii kutoka katika taasisi zinazotoa huduma ya kuypokea watalii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati huu wa janga la Corona wakifuatilia mada mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mafunzo ya utayari wa kupokea watalii  taasisi zinazotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati huu wa janga la Corona wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Balozi wa Ujereumani nchini Tanzania, Regina Hess mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hyayo  leo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimweleza jambo Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regina Hess wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utayari wa kupokea watalii watumishi wa taasisi zinazotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati huu wa janga la Corona leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Uchumi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA), Bw. Danny Mallanga ( kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utayari wa kupokea watalii watumishi wa taasisi zinazotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati huu wa janga la Corona leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa - WMU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.