Habari za Punde

PSSSF YAANZISHA HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO

Afisa Huduma kwa kwa wateja mwandamizi wa PSSSF, Bi. Nelusigwa Mwalugaja (kulia) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo

Na.Mwandishi Wetu, Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa kufika kwenye ofisi za Mfuko huo zilizoenea katika mikoa yote nchini ili kuhakiki taarifa zao.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es, Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe alisema mwanachama akifika kwenye ofisi yoyote ya PSSSF utaratibu na mahitaji yako vile vile hivyo amewahimiza kufanya hivyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kutohakiki taarifa.
Lakini pia amewaalika wanachama watakaotembelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere kwenye maonesho hayo ya biashara maarufu kama sabasaba, wataweza kujipatia huduma zote kama zinavyotolewa kwenye ofisi za Mfuko kwenye mikoa yote nchini.
“Tulichofanya mwaka huu tumehamisha miundombinu na vifaa vyote vya kutoa huduma vinavyopatikana kwenye ofisi zetu, hivyo mwanachama anapofika kwenye banda letu anapata huduma zote ikiwemo, taarifa za michango, mafao, pensheni na mafao yanayotolewa na Mfuko" alifafanua Bw. Mlowe.

2 comments:

  1. Ivi inakuaje mteja alijaza form za fao la uzazi akalipeleka psssf wakamkatalia nakumjibu adi apeleke mwajili. Akalipeka huko namwajili akapeleka hofisi

    ReplyDelete
  2. Habarini mbona fomu ya fao la uzazi hatuipati mtandaoni

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.