Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Ahudhuria Maziko ya Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin Mkapa Kijijini Kwao Lupaso Mtwara.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassima Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, wakijumuika katika hafla ya maziko ya Rais Mstaaf wa Tanzania Hayati Benjamin Willian Mkapa, yaliofanyika Kijiji kwao Lupaso Mkoani Mtwara 29-7-2020
VIONGOZI Wakuu wa Kitaifa wakiwa katika jukwaa maalum wakati wa hafla ya maziko ya Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa yaliofanyika 29/7/2020, kijiji kwao Lupaso Mkoani Mtwara.
VIONGOZI wa Jukwaa kuu la Viongozi wakiwa katika ibada ya kumuombea Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapa yaliofanyika Kijijin kwao Lupaso Mkoani Mtwara 29/7/2020,
ASKOFU Mkuu wa TUNDURU –Masasi Askofu Filbert Mhasi akiongoza Ibada ya maziko ya Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa yaliofanyika Kijijini Kwao Lupaso Mkoani Mtwara,
 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.