Habari za Punde

WanaCCM watakiwa kuridhika na maamuzi ya vikao vitakavyowajadili

Na Takdir Suweid                                             
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi wametakiwa kuridhika na maamuzi yatakayotolewa na Vikao mbalimbali vya kuwajadili.
Amesema Chama Cha Mapinduzi bado hakijasimamisha kumpata Mgombea wa Ubunge,Uwakilishi na Udiwani bali kilichofanyika ni kupiga kura ya Maoni ya kutoa muongozo wa Kiongozi atakae kiwakilisha Chama hicho.
Akifunguwa Mkutano wa kuchaguwa Madiwani wa Viti maalum Wilaya ya Dimani Kichama huko Kiembesamaki Katibu wa Umoja wa Wanawake (Uwt) Mkoa wa Magharibi Zuweina Suleiman Ali amesema vikao ndivyo vitakavyoamua Mgombea anaekubalika.
Amesema kuna baadhi ya Wanaccm wanatumiwa vibaya na baadhi ya Wagombea ambao kura zao hazikutosha kuongoza katika kura ya maoni jambo ambalo ni kinyume na maadili katika Uongozi.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi  Fatma Ramadhan Mandoba amewakumbusha Viongozi kushirikiana na kuzingatia maadili ya Chama ili kuzidi kukipatia Ushindi Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oct,Mwaka huu.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uwt Wilaya ya Dimani kichama wamewachaguwa Maryam Maboga,Riziki Ramadhani Kibweni,Venika Pangras,Maryam Saleh Ali,Salama Bakari Wakati na Shamila Jumbe Saidi kuwa Madiwani wa Viti maalum katika Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.