Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Burudi Jenerali Alaian Guillaume Ameondoka Nchini Baada ya Kuwasilisha Salamu za Pole Kufuatia Kifo Cha Mkapa.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume (Kulia) wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, muda mchache kabla ya Waziri Mkuu wa Burundi leo Julai 29, 2020 kuondoka nchini baada ya kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais na Wananchi wa Jamhuri ya Burundi  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na watanzania kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa . 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiagana  na Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam wakati  Waziri Mkuu wa Burundi leo Julai 29, 2020 akiondoka nchini baada ya kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais na Wananchi wa Jamhuri ya Burundi  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na watanzania kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa .
                                                           (Picha na Eliud Rwechungura)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.