Na Prisca Ulomi, WUUM, Arusha
Serikali yaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo
la ghorofa 17 za ofisi ya Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU)
unaoendelea kufanyika Mkoani Arusha
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano),
Dkt.Zainabu Chaula ambapo jana alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo mkoani humo akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Serikali na
PAPU akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary
Makondo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu Msaidizi wa
PAPU, Kolawole Aduloju, na watendaji wengine wa Halmashauri ya Jiji la Arusha;
na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Dkt. Chaula amesema kuwa ujenzi wa ofisi
za PAPU utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 33.7 na ni mradi wa kimkakati na wa kibiashara nchini hususan kwa biashara ya posta nchinia mbapo inategemewa kukua kupitia mradi huu ambapo lengo
la Serikali ni kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kukua zaidi kiuchumi na posta ni sehemu ya mkakati na ndio maana tunapitia mradi huu kila wakati ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa vizuri.
Ameongeza kuwa Serikali imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na inahimiza matumizi ya TEHAMA, Shirika la Posta Tanzania (TPC)
linatumia magari kutoa huduma zake kwa wateja ambapo moja ya jukumu lake ni
kufanyabiashara hivyo TPC anatumia biashara mtandao kwa kuingia makubaliano na muuzaji na mnunuzi wa bidhaa kutoka nchi yeyote na zinakuja
Tanzania na TPC anakuwa msafirishaji mkuu,
hii ni fursa na ni jukumu langu kuhakikisha mawasiliano haya yanaendelea kukua hususani kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
Naye msimamizi wa ujenzi wa jengo la
PAPU, Mhandisi Hanington Kagiraki amesema kuwa jengo hili litakuwa na ghorofa 17 na ujenzi
wake unagharamiwa kwa pamoja baina ya PAPU na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambapo hadi sasa kazi ya ujenzi na usimikaji wa nguzo za kujenga ghorofa 17
umefikia asilimia 75 ambapo jumla ya nguzo 145 zimezikwa kati ya nguzo 192
zinazohitajika kujengwa na mradi huu ni wa kipindi cha siku 900 na umeanza mwezi wa Januari
2020 na utakamilika mwaka 2022.
Katibu Mkuu Msaidizi wa PAPU,
Kolawole Aduloju amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa ushirikiano katika kujenga jengo hili na ujenzi unaendelea na wanaamini kuwa utakamalika kwa wakati
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary
Makondo amesema kuwa Serikali imenufaika kwa kupata ardhi ili mradi huu uweze kutekelezwa na hadi sasa vijana
70 wamepata ajira na tunatarajia watanzania na wana Arusha wataendelea kupata ajira.
No comments:
Post a Comment