Baadhi ya wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wakiwa katika mafunzo ya vitendo yaliyoandaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar .
Na Jaala Makame Haji---ZEC
Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya
jimbo walioteuliwa kusimamia Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi ya Zanzibar
kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia Sheria na maelekezo waliyopewa na Tume.
Mjumbe
wa Tume hiyo Dk. Kombo Khamis Hassan alitoa ushauri huo wakati akifungua
mafunzo ya siku tatu kwa Wasaidizi wasimamizi wa uchaguzi kwa Majimbo ya Unguja
yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni jijini
Zanzibar.
Dk
Kombo alisema Tume imekuwa ikiendelea kuchukua juhudi mbali mbali za
kuwakutanisha Wadau wa uchaguzi wakiwemo Vyama vya Siasa, Waandishi wa habari,
Asasi za Kiraia na Wadau wa kutoka katika makundi yenye mahitaji maalum kwa
lengo la kuona uchaguzi wa mwaka 2020 unafanyika kwa kufuataa misingi ya
Kidemokrasia na kudumisha Amani na utulivu hata baada ya Uchaguzi.
Akifunga
Mafunzo hayo Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Kanali Mstaafu Fetehe Saad
Mgeni aliwataka Wasimamizi wa uchaguzi na Wasaidizi Wasimamizi kuhakikisha kila
mwenye haki ya kuchagua na kuchaguzliwa anapata haki yake ili kuweka mustakbali
mzuri wa uchaguzi.Mkuu wa mwaka 2020.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Sheria Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Khamis Issa Khamis
alisisitiza kuwa kazi za Uchaguzi zinahitaji umakini wa hali ya juu kati hatua
zote muhimu ikiwemo hatua ya ujazaji wa fomu za matokeo ya Uchaguzi, utunzaji
wa vifaa, kuhesabu kura na kutangaza matokeo.
Ndugu
Khamis alifafanua kuwa Sheria ya Uchaguzi Namba 4 ya mwaka 2018 imeeleza makosa
na adhabu kwa atakaye kwenda kinyume Sheria hizo na aliwasihi wasaidizi wasimamizi wa Uchaguzi
pamoja na Watakao pewa jukumu la kusimamia uchaguzi katika vituo vya kupigia
kura kuzingatia zaidi Sheria za Uchaguzi ili kuepuka kuingia hatiani kwa mujibu
wa Sheria.
Mkuu
wa kurugenzi ya Elimu ya Wapiga kura, habari na Mawasiliano ya Umma Juma Sanifu
Sheha alieeleza kuwa ZEC katika kuwaondolea usumbufu watu wenye mahitaji maalum
wakiwemo watu wenye ulemavu imeandaa mikakati maalum ambayo itawawezesha kupiga
kura wenyewe na kuingia katika vituo vya kupigia kura bila kukaa foleni.
Ndugu
Sanifu alieendelea kusema kuwa, ZEC inatekeleza maelekezo ya Sera ya jinsia na
ushirikishwaji wa makundi maalum ya mwaka 2014 iliyoanzishwa na Tume hiyo ili
kuondosha usumbufu kwa makundi yenye mahitaji maalum wakiwemo Wanawake wanao
nyonyoshe, watu wenye ulemavu, Wazee na Wajawazito.
Akieleza
kuhusu upigaji kura kwa Watu wasioona alifafanua kuwa, Tume itaanda kifaa
maalum cha Kupigia Kura kwa Watu wasioona (Tactile Ballot Folder) chenye
maandishi ya nukta nundu ili nawao waweze kupiga kura wenyewe bila msaada wa
mtu mwengine.
Msaidizi
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo Chwaka Wilaya ya Kati Mwanajuma Khalfan Machano
mara baada ya kula kiapo cha utekelezaji wa majukumu yake katika ukumbi wa
Sheikh Idrisa Abdul Wakil kikwajuni jijini Zanzibar aliahidi kufuata na
kutekeleza taratibu zote walizoelekezwa na tume kupitia sheria na kanuni za
uchaguzi.
Naye
Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shauri Moyo Wilaya ya Mjini Hashim Ali
Suleiman alisema matarajio yao ni kuifanya kazi hiyo kwa uhuru na uwazi ambapo
aliwataka wananchi kushiriki uchaguzi katika hatua zote za uchaguzi kutokana na
Tume ya uchaguzi imejipanga kutoa huduma bila ya usumbufu wowote.
Mafunzo
hayo ya siku tatu yalifanyika Unguja na Pemba ambayo yalifunguliwa tarehe 22/8/2020 na kufungwa tarehe
24/8/2020.
No comments:
Post a Comment