Habari za Punde

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Wakisherehekea Ushindi Wao Maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Serikalini  Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Dorina Makaya (wa pili kushoto) na Meneja Msaidizi Kanda ya Kati, Patricia Manonga ( wa tatu kulia), wakiwa na baadhi ya  watumishi wa wizara hiyo, Taasisi na vyuo wakisherehekea ushindi walioupata baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa kwanza katika kundi la sekta ya uchumi na uzalishaji wakati wa kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia maswala ya Walemavu mhe. Stella Ikupa ( wa kwanza kulia) akimkabidi cheti kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Serikalini Bi. Dorina Makaya  (mwenye T-shirt nyeupe) na Bi. Patricia Manonga (wa kwanza kushoto) kwenye halfa ya kilele cha Maonesho ya Nane Nane  jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Serikalini Bi. Dorina Makaya (kulia) na Mratibu wa Maonesho ya Nane Nane (kushoto) wakiongoza wadau kuingia banda la wanyama kwenye Maonesho ya Nane Nane  jijini Dodoma.
(Picha Zote na Richard Mwaikenda 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.