Habari za Punde

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim Asisitiza Mashehe Waendeleze Kuhubiri Amani Nchini.

Waziri wa Katiba na Sheria  Zanzibar Khamis Juma Maalim akifungua mafunzo ya siku moja kwa Maimamu wa Mkoa wa Kaskazini juu ya Amani na Utulivu katika Ukumbi wa Ofisi ya Mufti Mazizini Zanzibar.
Sheikh Khamis Abdul-hamid akisisitiza Amani katika semina ya siku moja kwa Maimamu wa Mkoa  wa Kaskazini Unguja  iliyofanyika Ofisi ya Mufti Mazizini Zanzibar 

Katibu wa Mufti Khalid Mfaume akizungumza na Maimamu wa Mkoa wa Kaskazini (hawamo pichani) katika semina ya siku moja kuhusu Amani na Utulivu hafla  iliyofanyika Ofisi ya Mufti Mazizini Zanzibar .
Naibu Kamishna wa Polisi Afande Mpinga Gyumi akinukuu kifungu cha sheria ya uchaguzi katika kulinda amani wakati akiwasilisha mada ya wajibu wa kutii sheria bila kushurutishwa katika semina ya siku moja juu ya Amani na Utulivu kwa Maimamu wa Mkoa  wa Kaskazini Unguja huko Mazizini Zanzibar .

Maimamu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifatilia kwa kina semina ya Amani na Utulivu iliyofanyika ofisi ya Mufti Mazizini Zanzibar .

PICHA NA FAUZIA MUSSA/MAELEZO.
 


Na Ali Issa Maelezo 30/9/2020

Waziri wa katiba na sheria  Zanzibar, Khamis Juma Mwalim amesema viongozi wa dini wanawajibu wa kulinda na kuendeleza amani iliopo nchini kwa kutumia nafasi zao vyema kwa kuzungumza na waumini wao mara kwa mara.

Waziri huyo aliyasema hayo  huko Ofisi ya Mufti Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Maimamu, masheikhe na Makhatibu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema kikawaida mashekhe,maimamu na Makhatibu hukutana kila siku na waumini wao katika sala za pamoja kwa lengo la kuhabarishana masuala ya Dini na Imani, hivyo ni vyema kutumia vikao hivyo kwa kuwapa elimu zaidi waumini  juu ya kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani.


Alisema kufanya hivyo si faida kwa jamii pekee bali ni kwa Taifa zima hasa na kuwezesha nchi kupata sifa nzuri kwa wenyeji na wageni wanaofika kwa ajili ya kufanya ziara mbali mbali za matembezi. 

“Amani ni neema inayo toka kwa Allah tuilindeni mashekhe kwakutumia misikiti na mikusanyiko ya madras ili kuituza tunu hii ya taifa isitoweke”,alisema Waziri Khamis

Aidha waziri huyo alisema kuwa viongozi hao waendelee kuiombea dua nchi na kuufikisha ujumbe huo katika misikiti na majumba yao binafsi kulilizungumzia neno la amani na utulivu.

Nae mjumbe wa Baraza la Maulamaa Mkoa wa Kaskazini Shekhe Khamis Abdull akitoa mada juu ya wajibu wa Uongozi wa Dini katika kuimarisha amani ya Nchi alisema waislamu wote ni ndugu haifai mtummoja kumuumiza mwezake kwa kumsababishia maumivu au kumtia hofu kwa kumtisha na iwapo atafanya hivyo atambuwe wazi kuwa wanakwenda kinyume na mafundisho ya Dini yao.

Alisema kila mtu kwa dini yake, rangi,utaifa kabila na wakiwemo wanyama haipaswi kufanyiwa uadui kwani kila mmoja anahitaji apate raha hivyo utapomfanyia uaduwi tambua wazi amani hiyo itatoweka .

Alifahamisha kuwa binadamu wapendane na wasichukiane kwani maisha baada ya uchaguzi yataendelea na isiwe sababu uchaguzi ikawa ndio njia ya kudhulumiana na kuoneana.

Nae Shekhe Bakar Batwashi akitoa maada juu ya Amani katika nyumba za Ibada alisema Msikiti ni pahala pa Amani na Utulivu ndio maana anae ingia nyumba hiyo huwa yuko nadhifu  anapendeza kwa usafi na upole.

Alisema maimamu wazungumzie hisia za waumini na wajue kuwa wao ni viongozi walio aminiwa wanapaswa kutoa elimu inayo lingana na agizo la viongozi wakuu wa Nchi.

Mapema katibu wa Mufti Khalid Mfaume akimkaribisha Mgeni Rasmi alisema kuwa wamewaita makhatibu,Mashekhe na maimamu kubadilishana mawazo na kuzungumzia juu ya suala la amani na utulivu katika maeneo yao ya misikiti,madrasa na vyuo.

Aidha alisema mkutano huo utaendelea kwa masheikhe wa mkoa wa kusini na mkoa wa Mjini magharibi kuwapa mafunzo kamahayo walio ya toa  kwa viongozi hao.

Mkutano huo ulizungumzia mada kuu tatu Wajibu wa viongozi wa dini,wajibu wa Amani katika njumba za Ibadan a Utii wa sheria bila shuruti katika hali ya upigaji kura vituoni.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.