Habari za Punde

MAJALIWA AMTUMBUA MKURUGENZI MKUU WA MAGHALA, ODILO MAJENGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi , Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Wizara za  TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika, Mtendaji Mkuu wa  Bodi ya Korosho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya  Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala na Waendesha Maghala wote wa Mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi na Ruvuma kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 28, 2020. Katika Kikao hicho Mheshimiwa Majaliwa alitoa Maagizo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kumuondoa kwenye nafasi yake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala, Bw. Odilo Majengo kwa kushindwa kutii maagizo ya viongozi wa juu wa serikali kusimamia kuondoa tozo ya unyaufu kwenye zao la korosho
Baadhi ya washiriki wa Mkutano kati ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na   Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi , Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Wizara za  TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja na Mrajisi wa Ushirika, Mkurugenzi Mkuu wa  Bodi ya Korosho, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya  Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Mkurugenzi  Mkuu wa Bodi ya Maghala na Waendesha Maghala wote wa Mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi na Ruvuma  wakimsikiliza Mheshimiwa Majaliwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.