Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefanya Uteuzi leo 4/11/2020.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyiamemteua Bwana Suleiman Ahmed Salum kuwa Katibu wa Rais.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kabla ya uteuzi huo Bwana Suleiman Ahmed Salum alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.

Uteuzi huo ameufanya Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Wakati huo huo, Rais Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 6(1) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya mwaka 1997, amemteua Bwana Nahaat Mohammed Mahfoudh kuwa Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Nahaat Mohammed Mahfoudh amefanya kazi katika Taasisi mbali mbali za sekta binafsi

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 04 Novemba, 2020.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.