Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akisikiliza kwa makini wakati alipokutana na uongozi wa Step Up Foundation walipofika Ofisini kwake Chukwani.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Step Up Foundation walipofika Ofisini kwake Chukwani.
Na Mwandishi wetu
Spika wa Baraza
la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid ameishauri jamii
na taifa kwa jumla kuangalia namna bora zaidi ya kusaidia watoto wanaoishi
katika mazingira magumu hasa walioathirika na maambukizo
ya maradhi ya ukimwi.
Amesema hali
na namna wanayoishi Watoto hao ambao wamehifadhiwa katika vituo kadhaa binafsi kwa
ajili ya kusaidiwa, hairidhishi na haiko rafiki katika upatikanaji wa huduma
bora hasa wale walioathirika na maambukizo ya maradhi ya ukimwi kutoka kwa
wazee wao.
Mhe. Zubeir
ameeleza hayo ofisini kwake Chukwani wakati alipokuwa na mazungumzo na uongozi wa jumuiya ya maendeleo ya baadhi
ya wake wa viongozi wastaafu inayosaidia Watoto yatima .
Amesema
baadhi ya taasisi binafsi zimeonekana kuwa tayari kusaidia katika upatikanaji
wa huduma bora kwa watoto hao lakini ipo
haja kwa serikali kubuni mbinu bora Zaidi za kuisaidia ili kuwawezesha watoto
hao kupata haki yao ya huduma zinazostahili.
Nae Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Step Up
Foundation inayosaidia Watoto yatima mama Asha Balozi, amewataka wajumbe wa
baraza la wawakilsihi kuwa tayari kuchangia katika upatikanaji wa huduma zikiwemo
za elimu ili kuwasaidia Watoto wanaoishi katika mazingira magumu .
Kwa mujibu wa
utafiti mdogo wa hivi karibuni wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Stepup Foundation inayosaidia Watoto yatima, zaidi ya wototo elfu 57
waliosajiliwa ni mayatima na wanaishi katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment