Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aendelea na ziara yake kisiwani Pemba akagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi Mfikiwa, Kusini Pemba

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (aliyevaa tai), akikagua matofali ya Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi, zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo leo, lengo ikiwa ni kutatua makazi ya askari hao.Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi  Zanzibar, Mohammed Haji Hassan.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, akipita mbele ya nyumba za askari polisi(zinazoonekana pichani) zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba ambazo zilijengwa na fedha zilizotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ikiwa ni mkakati maalumu wa kutatua changamoto za makazi ya askari nchini.Kulia  ni Kamishna wa Jeshi la Polisi  Zanzibar, Mohammed Haji Hassan.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akiteta jambo na Kamishna wa Jeshi la Polisi  Zanzibar, Mohammed Haji Hassan(kulia)leo  wakati wa ziara ya ukaguzi  wa  Mradi wa Ujenzi wa  Nyumba za Makazi ya Askari Polisi, zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan (wapili kushoto),akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara ya ukaguzi  wa  Mradi wa Ujenzi wa  Nyumba za Makazi ya Askari Polisi,leo  zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.