Habari za Punde

Skuli Kufunguliwa tarehe 18/01/2021


                               TANGAZO MAALUM.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hija, anawatangazia walimu, wazazi na wanafunzi wote kuwa Skuli zote zitafunguliwa tarehe 18/01/2021.
Pia Wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha pili wanatakiwa na wao kuripoti Skuli siku hiyo na walimu wawaingize kidato cha TATU.
Yakitoka matokeo kwa wanafunzi waliofaulu wataendelea na kidatu cha TATU na waliofeli watarudia kidatu cha pili.
Hivyo walimu wakuu wote mnatakiwa kuwajua wanafunzi wote wasiofanya mtihani na sababu zao ziwe za msingi ili Wizara ikichukua hatua iwe na takwimu sahihi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.