Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita alisema anataka wasimamizi wa viwanja wahakikishe wafanyakazi wanapatiwa vitendea kazi vya kisasa, vigari vya kufyekea, ofisi na upatikanaji wa maji muda wote. zungumzeni na ZAWA ili suala la maji hasa ya kunywa lipatiwe ufumbuzi.
Nisisitize Mipango yote ambayo imepangwa na Wizara ya kukiboresha kiwanja cha Mao ze dong ikiwemo ujenzi wa chumba cha kubadilishia nguo (changing room) ianze mara moja bila ya kusubiri ugeni wa wachezaji wa kimataifa.
Wafanyakazi wana dhamana kubwa ya kuvitunza viwanja vya michezo vidumu katika hali ya usafi ndani na nje. Kila mmoja atimize wajibu wake kwa mujibu wa nafasi yake ili sekta ya michezo iweze kuimarika.
Taa za chumba cha viongozi mashuhuri (VIP) katika kiwanja cha Amani zifanyiwe matengenezo ya haraka hakuna sababu ya kusubiria mpaka kuwe na vikao na sherehe ndio zitengenezwe.
Kikundi cha Sanaa ya taarab asilia lazima kifufuliwe ili kitumike katika shughuli mbali mbali za kitaifa sio kwenda kuvikodi vikundi vyengine vya sanaa.
No comments:
Post a Comment