Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar yapokea msaada wa vifaa vya Kinga kutoka UNDP

Meneja Uwendeshaji Shirika  la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) Jeremiah Mallongo akimkabidhi msaada wa Vifaa kinga   Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa jamii Jinsia na Watoto  Juma Salum Mbwana huko Wizara ya Afya Mnazimmoja  Zanzibar 

Na Rahima Mohamed  Maelezo Zanzibar. 2\12\2020        

Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto imepokea vifaa tiba kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambavyo vitasaidia  kukabiliana na maradhi ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Akikabidhi vifaa hivyo Meneja Uendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Jeremiah Mallongo katika Ofisi ya Wizara hiyo huko Mnazimmoja  amesema wanatambua juhudi kubwa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika kupanga , kuratibu na kutekeleza mpango wa tahadhari katika kukabiliana  na magonjwa hayo..

Amesema vifaa hivyo vitasaidia katika kupambana na kudhibiti maradhi ya kuambukiza ambayo yanarejesha nyuma soko na mfumo wa utalii na kudhorotesha biashara hiyo muhimu ya kukuza uchumi wa nchi.

Amesema vifaa hivyo vinathamani ya TZS millioni, 271,504,378 ambavyo vinajumuisha ICU Ventilators 4, Oxygen Concentrators 10, Respirators 2016, Examination Gloves 1000, Surgical Gowns 500 na Surgical Masks 4000 .

Aidha amesema shirika hilo litagharamia  ufungaji wa vifaa tiba vyote katika sehemu ambazo wizara itaamua vifungwe mara baada ya uainishaji wa maeneo hayo utakapofanyika.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambae pia Mkurugenzi Tiba wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto Juma Salum Mbwana amesema wamepokea  msaada wa vifaa hivyo na kuhakikisha watavitumia vizuri kwa lengo la kujikinga na magonjwa mbalimbali ili  wananchi waishi  katika hali ya salama na amani.

Aidha amesema vifaa hiyvo vitasaidia katika hali ya usalama kwa watalii watakao ingia nchini na kuwakumbusha kufuata taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha mikusanyiko inakuwa ya amani.

 Baadhi ya Vifaa kinga vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wizara ya Afya  .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa jamii Jinsia na Watoto  Juma Salum Mbwana  akitia saini hati ya makabidhiano msaada wa vifaa kinga mara baada ya makabidhiano huko  Wizara ya Afya Mnazimmoja  Zanzibar 
Meneja Uwendeshaji Shirika  la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) Jeremiah Mallongo  akitia saini hati ya makabidhiano msaada wa vifaa kinga mara baada ya makabidhiano huko  Wizara ya Afya Mnazimmoja  Zanzibar .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa jamii Jinsia na Watoto  Juma Salum Mbwana akitoa neno la shukurani kwa UNDP  mara baada ya makabidhiano ya Msaada wa Vifaa kinga hafla iliyofanyika   Wizara ya Afya Ustawi wa jamii Jinsia na Watoto Zanzibar .

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dr.Fdhil Abdalla akijibu maswali ya waandishi wa habara yanayohusiana na msaada uliotolew na  UNDP huko Wizara ya Afya Mnazimmoja  Zanzibar . 

PICHA NA FAUZIA MUSSA / MAELEZO ZANZIBAR.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.