Habari za Punde

KMKM yatoa wachezaji wake kucheza Tanzania Bara

 NA MWAJUMA JUMA

KLABU ya soka ya KMKM umewatowa wachezaji wake wawili kwenda kuchezea katika klabu za Tanzania Bara.

Wachezaji hao ni kiungo mshambuliaji Mateo Anthony ambae ameenda klabu cha KMC na Mwinyi Haji Mngwali 'Bagawai' ambae ameenda Ruby Shooting.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu msaidizi wa timu hiyo Suleiman Rajab Kisheta amesema taratibu za usajili kwa wachezaji hao tayari isipokuwa kea bagawai yeye bado kuna baadhi ya mambo hayajakamilika.

"Mateo tayari tushamalizana kila kitu na klabu yake anayokwenda kuichezea lakini kwa bagawai bado kuna vitu havijakamilika", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kutokana na kutoa wachezaji hao wawili na wao wanasubiri dirisha dogo ili kuweza kuongeza nafasi moja.

Alifahamisha kwamba mpaka sasa katika usajili huo wanatarajia kusajili nafasi ya mshambuliaji pekee.

"Tunasubiri dirisha dogo ili tusajili mchezaji mmoja tu na kea nafasi nyengine bado zipo sawa na tunaimani wataweza kuwa sawa", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa bado timu yao inaendelea kusaka ubingwa na msimu huu watajitahidi kuona mambo yanaenda Kama ambavyo wamepanga.

KMKM ambayo inashiriki ligi kuu ya Zanzibar inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 19 akifatiwa na Mafunzo wenye pointi 12.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.