Na, MOHAMMED SHARKSY
KUPOTOKA KWA NGONO (SEXUAL DEVIATION)
Kupotoka
kwa ngono (sexual deviation) ni janga
kubwa lilioikumba jamii yetu, rushwa ya muhali ndio kichocheo kikuu cha
ongezeko la kupotoka kwa ngono na unyanyasaji wa kijinsia.
Katika siku za
hivi karibuni kumetokezea kesi za uzalilishaji wa kijinsia hasa kutoka jamii ya kiume dhidi wanawake na watoto kiasi
ambacho kila uchao katika vyombo vyetu vya habari vinazungunzia matukio haya ya
uhalifu,mbali kwamba vyombo vya sharia
kama polisi na mahakama vinafuatilia kwa
ukamiliffu katika kutatua tatizo hili bado limekuw kidonda ndugu.
Makala hii Imeona
kuna umuhimu wa kuzungunguzia hali halisi ilivyo , hasa kutokana na chanzo chake kikuu huwa kinasabishwa na kupotoka kwa
ngono
Kupotoka kwa ngono
(sexual deviation) inawezeka ikawa ni laana inayofanywa na baadhi ya watu kutokana
na ujinga wa kutojitambuwa katika mzingira fulani au tunaweza kukasema ni ugonjwa
wa akili ambao mara nyingi unapoanza unaonekana ni hali
ya kawaida tu na huenda pasiwepo na jitihada yoyote ya kupata msaada
wa kimatibabu mpaka hali itakapokuwa mbaya au kuzidiwa
Ngono/tendo la ndoa ni ile hali ya
faraha ya kuonana kimwili baina ya mke
na mume ,ni zawadi maalumu kutoka kwa
Mungu inapofanywa katika ndoa kwa raha na bashasha tele ndani yake kukiwa na utulivyo katika moyo . Kufurahiana na kuonana kimwili
ni jambo la kutiliwa maanani katika ndoa.
Mungu aliumba hali ya kuonana kimwili
kuwa uhusiano katika ya mke na mume katika ndoa. Na ifahamike
kwamba kufanya tendo la ndoa
kinyume na maumbile ni haramu na
haikubaliki katika dini zetu zote,
NINI MAANA YA KUPOTOKA KWA NGONO KIAFYA?
Kupotoka kwa ngono ni ugonjwa wa akili
unaompata binadamu na kuifanya akili
yake iwe na matamanio kinyume cha fikra umri na uhalisia ulivyo.
AINA ZA KUPOTOKA KWA NGONO
Ziko aina nyingi sana za Kupotoka kwa ngono,
zifuatazo ni aina chache na maarufu sana
katika jamii zetu hasa katika hizi nchi za dunia ya tatu kama Zanzbar na T anzania kwa jumla.
Ø Kupiga
bodi (Voyerisim) , hii ni ile hali inayomfanya mtu kuchungulia madirishani au
kupanda kuta za majumbani mwa watu na kuchungulia watu wakiwa wamelala na
familia zao kwa lengo la kiujifurahisha na
kujisikia kwamba matamanio yake
yamekamilika
Ø Kuingilia
watoto wadogo kinyume na maumbile ya
kawaida. Hii humtokezea mtu mwenye umri mkubwa kwa kujitosheleza na matamanio yake kwa
kumuingilia mtoto
Ø Kusagana
(exhihibitionism).hii ni hali inayowafanya wanawake au wasichana wa umri mkubwa
kufanya tendo la mapenzi kwa kuchezeana
kwenye tupu zao ilimradi wajizirishe kuondowa hisia zao za mapenzi
Ø Kuingiliana
kwa wanaume kwa wanaume. Hii ni mila potefu ambayo hata katika dini zote zimeharamisha kitendo hichi lakini hufanywa
na baadhi ya wanaume ili kumalizia matamanio yao ya mapenzi
Ø Kubaka.
Hiki nikitendo cha kijinai kinacho fanywa na wanaume kumlazimisha kufanya tendo
la ndoa kwa kumuingilia mwanamke bila ya
ridhaa yake mwenyewe .
Ø Sexology; Ni wale wat u ambao wanjisikia kama kwamba wamefanya tendo la ndoa pale
wanpoonyesha jamii sehemu za siri bila ya aibu
bila kujali umri au rika ya mtu ilivyo .
Ø Zoophilia
wale watu wanajiridhisha hisia zao kwa kufanya
tendo la ndoa na wanyama
Ø Fetishism
ni wale watu ambao wanatumia vitu visivyokuwa na uhai kwa kufanya tendo la ndoa ili kujiridhisha,
mara nyingi hutumiwa sana na wanawake
kama bilingani, muhogo, ndizi nk.
Ø Frotteurisme
ni ile jamii ya watu wanojiridhisha wakihisi wamesha fanya tendo la ndoa
pale wanapo jigusanisha sehemu zao za
siri na mtu mwengine pindi ambao wamevaa nguo, hii sana huwa inatokezea kwenye
vyombo vya usafiri kama vile kwenye dala dala
pindi pale watu wanaposimama ,na hii hufanyika sana kwa wanaume.
Ø Masterbeshan/kupiga
beshion.Hii ni ile ya wanaume kusuguwa uume wake kwa milihaji ya kujitowa
shahawa/manii ili kujiridhisha kama vile amefanya tendo la ngono.
MATIBABU YA KUPOTOKA
KWA NGONO
Ø Kupatiwa
ushauri nasahaha kuhusiana na mambo ya
ngono salama na athari zake
Ø Kutumia
dawa za kemikali zinazozosaidia kupunguza vichochezi vya ngono (lutilizing
hormones releasing argonisting)
Ø Kuangalia
historia ya mgonjwa katika kumbukumbu ya
magonjwa ya akili katika familia
Ø Kuwashauri
watu kupunguza msongo wa mawazo na kuwa
huru kujieleleza kwa hali yeyoyte
Ø Kuwashajihisha
walengwa wa vitendo hivi kusoma vitabu
vitakatifu na kujuwa juu ya maamrisho na makatazo ya alwah.
MADHARA YA KUPOTOKA KWA NGONO.
Mara nyingi sana madhara ya kupotoka kwa
ngono yanawaelemea sana wanawake kuliko wanaume.
Ø Kuongezeka
kwa matukio ya udhalilishaji wa kijinsia .
Ø Wanawake kuathirika kwa magonjwa ya zinaa kama
vile Ukimwi,kaswende,kisonono, nk.
Ø Ufanyaji
wa mapenzi ya ngono potofu usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe na
msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri
kutowa ute unaoweza kuwakinga na michubuko na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta m
madhara makubwa katika uke wao.(hii nikutokana na kukosa ridhaa yake ya kufanya
tendo la ndoa)
Ø Kupotezea
haiba zao kwa jamii
Ø Kathirika
kisaikolojia
Ø Kupata
mimba sisizotararajiwa
Ø Kongezeka
kwa watoto wa mitaani.
Ø Kuparaganyika
kwa familia
Ø Kongezeka
kwa vifo vya wanawake visivyotarajiwa kama kujiuwa kwa makusudi kutokana
nakadhia ya kubakwa .
Ø Kuongezeka
kwa vifafa vya mimba kutokana na mimba za utotoni katika umri mdogo katika
miaka ya kumi mpaka kumi na tano.
Ø Kuongezeka
kwa wanawake tegemezi.
Ø Kupata
kwa maambukizi ya viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija
ya uzazi kwa ujumla wake kama tatizo la PID,(Pelvic Infamatory diseases tatizo
ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.
CHANGAMOTO
Akizungumza na mmoja kati ya Afisa Ustawi wa jamii wa Wilaya ambae hakutaka jina lake
kutajwa alizungumzia changamoto zinazowakabili
sana ni kwamba makosa mengi ya udhalilishaji wa kingono na kijinsia yanaongezeka kwa kasi
zaidi kwasababu zifuatazo kama vile ruchwa/rushwa ya muhali kwa wanafamilia na
wanajamii,kutowajibika kwa baadhi ya watendaji,kesi
kuchukuwa muda mrefu, kukosa imani ya kiroho,wazazi kutokuwa karibu na watoto
wao ,matumizi mabaya ya mitandao na mwisho kuondoka kwa malezi ya kizamani
USHAURI
Sio watu wote wanayofanya vitendo vya
udhallishaji wa ngono potovu kwamba wana makosa baadhi yao ni wagonjwa wa akili kwa hiyo serikali na jamii isichukulie kwa
urahisi katika kutowa maamuzi yake kabla ya uchunguzi yakinifu .na iwapo itakugundulika
na makosa hatua kali za kisheria zichukulie
zidi yao.
Imetayarishwa na:
Mohammed Sharksy .
Mkufunzi Msaidizi
Kutoka Skuli za Sayansi za Afya
Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, SUZA
0777432493 au email:
mohammed.rashid96@yahoo.com ruruma96@gmail.com
No comments:
Post a Comment