Habari za Punde

Bodi ya Wakurugenzi Tanesco Yatembelea Vituo vya Kufulia Umeme vya New Pangani Falls na Hale Korogwe Tanga.

Mhandisi Uzalishaji wa Kituo cha New Pangani Falls Dalali Lunyamila akiwaonyesha Wakurugenzi wa Bodi ya TANESCO namna Mtambo wa New Pangani Falls unavyofanya kazi wakati wa ziara yao.

MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Balozi James Nzagi amewataka wawekezaji nchini kuwekeza nchini kutokana na uwepo wa umeme wa kutosha na ziada ambao utawawezesha kuweza kufanya shughuli zao bila vikwazo vyoyote.

Balozi James aliyasema hayo wakati wa ziara ya bodi hiyo ilipotembelea vituo vya kufufua umeme vya New Pangani Falls na Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga na kujionea namna wanavyofanya kazi zao huku wakionyeshwa kuridhishwa na uzalishaji unaopatikana kwenye vituo hivyo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea vituo hivyo Balozi James alisema lengo la ziara yao ni kutokana na maagizo yaliyopewa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kwamba bodi hiyo itembelea vituo vyote vinavyozalisha umeme hapa nchini.

Alisema wamefika wameona na wamepata maelezo namna mitambo inavyofanya kazi na wao wameona ni muhimu mitambo inavyofanya kazi ili kujiridhisha umeme unaozalishwa unakuwa na kutosha na wameona umeme unaozalishwa hauna matatizo

“Pangani wanazalisha Megawati 68 kutoka kwenye mashine mbili ambazo kila moja inazalisha 34 na Hale wanazalisha Megawati 34 kwa hiyo tunachokiona umeme unapatikana wa kutosha hivyo wananchi asiwe na wasiwasi kwamba kutakuwa na upungufu wa umeme”Alisema Balozi James

Aidha alisema pia kuhusu wale wenye shughuli zinazohusiana na nishati ya umeme wafanya shughuli zao bila wasiwasi kutokana na uwepo wa umeme wa kutosha na zaidi uliopo hapa nchini .

Kuhusu umeme unazalishwa na maji alisema wametizama vyanzo vya maji New Pangani Falls kuna maji ya kutosha ingawa kuna haja ya kurekebisha bwawa ili kuwa na maji ya kutosha siku zote hivyo hawatakuwa na wasiwasi wa kupata tatizo la umeme kutokana mashine kutosimama na zinafanya kazi nzuri.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Meneja wa Pangani Hydro System Steven Mahenda alisema ili kuzuia tope lisiendelee kuwepo kwenye bwawa hilo wanataraji kufanya marekebisho kwenye bwawa hilo yatakayo saidia kuondokana na tatizo la bwawa kujaa tope na kupelekea kina cha maji kupungua.

Alisema pia watatengeneza miudombinu kabla ya maji kuingia kwenye bwawa kuwe na sehemu ambao kuna kama shimo maji yakifika uchafu unachujwa na mchanga ukijaa kwenye hilo eneo wanaondoa.

Hata hivyo alisema wameshapata kibali kutoka menejimenti ya TANESCO wanamtafuta mkandarasi na wamekisha kupelekea watu wa manunuzi imeshatangazwa inafanyaa tathimi ili kuweza kujuia ndani ya bwawa kuna tope kiasi gani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.