Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Amejumuika na Wananchi wa Zanzibar Katika Sala na Dua ya Kumuombea Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar. SAMIA AJUMUIKA NA WANANCHI WA ZANZIBAR KUSALIA NA KUAGA MAALIM SEIF

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi wa Zanzibar katika Sala Maalum ya Kusalia Mwili wa  aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliyosaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Mawaziri wa SMT na SMZ wakishiriki katika Sala ya kuusalia mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena A. Said  katika Viwanja vya Mnazi mmoja Zanzibar wakati wa Ghafla ya Kusalia na kuaga Mwili wa  aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Wananchi mbalimbali wa Zanzibar katika Viwanja vya Mnazi mmoja baada ya kumalizika kwa Sala Maalum ya Kusalia Mwili wa  aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliyosaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo Febuari 18,2021.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.