Habari za Punde

Uchaguzi mdogo jimbo la Pandani na Wadi ya Kinuni kufanyika Machi 28

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid akizungumza na wadau wa uchaguzi wadi ya Kinuni 

Na Jaala Makame Haji - ZEC

Tume ya Uchaguzi 
Zanzibar
 ZEC imesema katika Uchaguzi Mdogo wa 
Jimbo
 la Pandani na Wadi ya Kinuni unaotarajiwa kufanyika Mach, 28, 2021 hakutakuwa na Upigaji Kura wa Mapema kutokana na maelekezo ya Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Namba 4 ya mwaka 2018.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa 
Tume
 hiyo Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Wadi ya Kinuni uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kinuni.

Mheshimiwa Mahmoud alisema kuwa, Tume kwa kuzingatia maelekezo ya Sheria ya Uchaguzi imeamua kuwa tarehe 12 Machi, 2021 itakuwa ni siku ya uteuzi wa Wagombea kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa 
Jimbo
 la Pandani na Wadi ya Kinuni.

Naye Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mheshima Makame Juma Pandu aliwataka wadau wa Uchaguzi wakiwemo viongozi wa Vyama vya Siasa na Wapiga Kura kuendelea kushirikiana na Tume katika kukamilisha Uchaguzi Mdogo huo kama walivyoshirikiana kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa salama na Amani

Aidha Mheshimiwa Makame aliwaomba waandishi wa habari kuendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuitunza Amani ya nchi kabla, wakati na baada ya uchaguzi na kuachana na tabia ya kuchurusha taarifa ambazo zinaweza kuhatarisha Amani ya Taifa.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo Kaimu Mkuu wa kitendo cha huduma za Sheria Mbaraka Said Hasuni aliwataka wadau wa Uchaguzi kuzingatia vifungu vya Sheria ili kuepukana na Makosa ya Uchaguzi yaliyoanishwa katika Sheria ambayo yataweza kuwaletea usumbufu siku ya uteuzi wa Wagombea.

Alisema, mgombea anatakiwa kuzingatia Zaidi kuwa, saa ishirini nan ne (24) baada ya muda wa mwisho wa urejeshaji wa fomu zitatumika kuweka wazi fomu za wagombea katika eneo la wazi la ofisi ya Tume ya uchaguzi ili kutoa nafasi kwa wagombea kuweka pingamizi ambapo pingamizi za uteuzi zitawekwa ndani ya muda huo wa saa 24 na ada ya pingamizi za uteuzi ni shilingi elfu Hamsini 50, 000 za Kitanzania.

Uchaguzi Mdogo wa Wadi ya Kinuni utafanyika sambasamba na Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Pandani tarahe 28 Machi, 2021 ambapo uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi utanza tarehe 03 Machi 2021 mpaka 11 Machi, 2021 na tarehe 12 machi itakuwa ni siku ya uteuzi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.