Habari za Punde

Uzinduzi wa kampeni maalum ya usafi kwa maendeleo ya Utalii.Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa akishirikiana  na wadau mbalimbali katika zoezi la usafi  kisiwani Kwale Zanzibar katika uzinduzi wa  kampeni maalum ya usafi kwa maendeleo ya Utalii.
Msanii maarufu  Zuhura Othman Soud (ZUCHU) kushoto akishiriki katika zoezi la usafi Kisiwani Kwale Zanzibar.
Baadhi ya Vijana wa Mjini Unguja  wakishiriki katika zoezi la  usafi kisiwani kwale Zanzibar katika uzinduzi wa  kampeni maalum ya usafi kwa maendeleo ya Utalii.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa akitoa neno kwa  wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya Usafi kwa Maendeleo ya Utalii baada ya kushiriki zoezi la usafi wa  Kisiwa cha Kwale Zanzibar.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa (kulia) akimkabidhi cheti maalumu Balozi Mteule wa Utalii Zanzibar Zuhura Othaman Soud (ZUCHU) katika uzinduzi wa kampeni maalum ya Usafi kwa Maendeleo ya utalii katika kisiwa cha  Kwale Zanzibar.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa  (kulia)  akimkabidhi cheti maalum Mama Zuchu Khadija Kopa katika uzinduzi wa kampeni maalum ya Usafi kwa Maendeleo ya utalii  huko Kwale   Zanzibar.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa  (kulia) akimkabidhi   cheti maalum mwakilishi kutoka Safari Blue  katika uzinduzi wa kampeni maalum ya Usafi kwa Maendeleo ya utalii  huko Kwale   Zanzibar

 Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa  (kulia) akimkabidhi   cheti maalum mdhamini wa uzinduzi wa kampeni ya usafi kwa maendeleo ya utalii kutoka kampuni ya  Camel Wheat Flours Meels katika kisiwa cha  Kwale Zanzibar.


  Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa  (kulia) akimkabidhi   cheti maalum mwakilishi wa Red Cross katika  uzinduzi wa kampeni maalum ya Usafi kwa Maendeleo ya utalii katika kisiwa cha  Kwale   Zanzibar.


Na Rahima Mohamed          Maelezo  

Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Mh Lela Mohamed Mussa amewataka wakuu wa Wilaya kuanzisha siku maalum kwa ajili ya kusafisha vivutio vya utalii .

Hayo ameyasema katika uzinduzi wa kampeni ya usafi kwa maendeleo ya utalii katika kisiwa cha Kwale Mkoa Mjini Magharibi siku hiyo maalum ya siku ya usafi itakuwa inafanyika kila baada ya mwezi mmoja ikiwa ni muendelezo wa usafi huo ili kupambana na taka na uharibifu wa mazingira unaopelekea vivutio hivyo kukosa haiba kwa wageni wanoingia nchini.  

Vilevile amezitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo uchafu katika vivutio vya utalii ikiwemo Mji Mkongwe,fukwe ,visiwa na maeneo ya  biashara ambazo watalii huhudumiwa .

Amesema uchafu katika maeneo ya utalii hupelekea kupoteza haiba ya mji wa kitalii wa Zanzibar. na kuhatarisha usalama wa afya  kwa wageni hasa katika usalama wa vyakula majiani.

“Uchafu katika maeneo unaweza kuhatarisha usalama wa afya kwa wageni hasa wale wanaopata huduma ya vyakula njiani inabidi usafi uzingatiwe na kuwekwa mazingira safi kwa wauzao vyakula hivyo”,alisema Waziri huyo.

Aidha alisema hali inayosababishwa na utupaji ovyo wa taka unaochochewa na uduni na utaratibu wa utekelezaji sera na sheria za usafi  wa mji  katika maeneo ya kitalii.

Pia Waziri huyo amewataka halmashauri  ya Magharibi B kusimamia na  kuhakikisha visiwa vinakuwa safi na waendane na tozo wanazowatoza wafanya biashara ya utalii.

Aidha amesema Zanzibar ni moja ya visiwa vichache vilivyofaidika kupitia biashara ya utalii ambao ni sekta mama inayochangia  uchumi wa nchi kwa asilimia 30.

Aidha waziri huyo  ameipongeza jumuiya Zanzibar Impowerment Organization  (LEO) pamoja na wadhamini wengine kwa kufanikisha kampeni ya usafi katika vivutio vya utalii ambayo itakua endelevu nchi nzima kwa  kuendeleza na   kuunga mkono jitihada za Uchumi wa bluu.

Nae Katibu wa Zanzibar Impowerment Organization Fatma Sarahani amempongeza Waziri wa Utalii kwa kuwaunga mkono kukubali kuzindua mradi huo ambao utawasaidia vijana kutatua changamoto za ajira pamoja na kuviweka safi vivutio vya utalii .

Amesema kwa kutumia fursa zilizopo wamebuni   miradi maalum na kuaanda mikakati ya muda mrefu na mfupi   kwa lengo la kuwatafutia ajira katika maeneo yao wanayishi ili kufaidika na sekta ya utalii.

Amesema mradi huu wa usafi katika sekta ya Utalii ni  mkubwa sana ambao utarejesha matumaini ya vijana wengi na kuleta muamko mpya na muuendelezo wa utalii  visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.