Na.Raya Hamad – OMKR .
Watendaji wa Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais wametakiwa
kuendeleza mashirikiano kiutendaji kwa lengo la kutekeleza vyema majukumu malengo na matarajio ya Serikali kwa kuzingatia
maagizo aliyoyatoa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe
Dkt Hussein Mwinyi
Waziri wa nchi Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya ameyasema hayo mara baada ya
makabidhiano ya Ofisi hio na aliyekuwa
Kaimu Waziri Dkt Khalid Salum Mohamed ambae
ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Uratibu wa
shughuli za Baraza la Wawakilishi
Serikali ya awamu ya
nane inadhamira ya kuondosha kero
zinazowakabili wananchi hivyo atahakikisha malengo hayo anayatimiza kwa mashirikiano ya pamoja na wakuu wa Taasisi zote na wafanyakazi
katika kuwatumikia wananchi na kuleta
maendeleo ya jumla
Dkt Saada amewaomba
wafanyakazi kuendelea kumuombea dua aliekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais marehemu
Maalim Seif Sharif Hamad aliefariki Febuari 17 mwaka huu ambae aliacha msingi
mzuri wa majukumu ya Ofisi hio na jamii kwa ujumla
Akizungumzia
changamoto zinazoikabili Ofisi hio Dkt Saada amesema ni muhimu kuangalia mapungufu yaliyopo na
kuyapatia ufumbuzi ikiwemo wafanyakazi kupata stahiki zao, kuandaa utaratibu wa
kuyalipa madeni pamoja na kuziangalia namna bora ya kuzipitia sheria
‘tuhakikisha
tunasimamia stahiki za wafanyakazi ila niwaombe sana wakuu wa taasisi kuwafahamisha wafanyakazi kutofanya kazi kwa
mazowea au kupitia migongo ya wengine kwani
wapo baadhi ya wafanyakazi hawana ari ya kiutendani hivyo wajiandae maana tunataka kuona vipi mshahara
wake anautendea haki kiutendaji’
alisisitiza Dkt Saada
Aidha Mhe Saada
amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais inasimamia masuala mtambuka hivyo
wakuu wa Taasisi wanawajibu wa kusimamia vyema vyanzo vya mapato na kuchangia ukuwaji wa uchumi kama
ilivyokusudiwa
Nae Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais, Uratibu wa shughuli za Baraza la Wawakilishi Dkt Khalid
Salum Mohamed ambae alikuwa akikaimu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amewashukuru
watendaji na wafanyakazi wote na kuwataka kumpa mashirikiano Mhe Saada ili
aweze kutekeleza vyema majukumu yake
Akitoa shukurani kwa
niaba ya watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mkurugenzi kutoka
Mamlaka ya Mazingira ndugu Sheha Juma Mjaja wameahidi kumpa mashirikiano na
upendo katika utekelezaji wa majukumu ya kazi na kuhakikisha ofisi inakwenda
sambamba na dhamira ya Serikali ya kuitumikia jamii
Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais inatekeleza majukumu yake
kupitia Ofisi ya faragha, Idara ya mipango Sera na utafiti, Idara ya Uendeshaji
na Utumishi , Idara ya mazingira, Idara ya Watu wenye Ulemavu, Mamlaka ya Mazingira, Tume ya Ukimwi, Tume ya
Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya na Afisi Kuu Pemba ambapo inawafanyakazi 306 Unguja na Pemba kati yao 156 wanawake na 150
wanaume .
No comments:
Post a Comment