Habari za Punde

Vijana wa Kisiwani Pemba Waadhimisha Siku ya Urithi Duniani Kwa Upandaji wa Miti

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa akizungumza nba Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati wa zoezi la Kuadhimisha Siku ya Urithi Duniani kwa upandaji wa miti katika Kijiji cha Maziwangombe Pemba, nakushoto Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba Mhe. Mohammeed Mussa Mkobani.

Na.Mwandishi Wetu Pemba.
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa amewataka  vijana kuimarisha utamaduni wa kupanda miti hasa sehemu za historia  ili   kizazi cha baadae kije kurithi  matunda sambamba na kuongeza vivutio vya utalii Kisiwani Pemba.

Akizungumza baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti huko Maziwangombe wilaya ya Micheweni ikiwa ni madhimisho ya siku ya urithi duniani Mhe Lela amesema vijana kupitia siku hiyo wanapaswa kuendeleza  kupanda miti na kuthamini maeneo yenye historia  ili kuweza  kuibua  vivutio vingi vya Utalii Kisiwani Pemba katika kusaidia kuondoa changamoto ya ajira kwa Vijana.

Mapema Afsa Mdhamini wa Wizara ya Utalii na mambo ya kale Pemba Bi.Zuhura Mgeni Othman  amesema   wizara  itaendelea kushirikiana na vijana ili kuifanya Pemba kuwa Kisiwa cha kijani huku  Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe.Mohamed Mussa Mkobani ameahidi kuwachukulia hatua watakaohusika na kuharibu miti iliyopandwa

Kwa upande wake Ndg. Haji Seif  Yusuph Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi na Urithi Pemba amesema  wanaendelea kushajihsha jamii kupanda miti katika maeneo yanayowazunguka pamoja na kuziimarisha sehemu za utalii ili ziendelea kuchangia kipato cha Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.