Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Amejumuika na Wananchi Katika Futari Aliowaandalia Katika Viwanja vya Nyumbani Kwake Maisara.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman akijumuika na Wananchi na Viongozi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Aliyani baada ya kumaliza Sala ya Magharibi iliofanyika katika viwanja vya  nyumbani kwake Maisara na (kulia kwake) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh,Saleh Omar Kabi. wakati wa hafla ya futari aliyowaandalia Wananchi na Viongozi.  
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wakijumuika na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman iliofanyika katika viwanja vya nyumbani kwake Maisara Jijini Zanzibar. 
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika katika futari maalum ilioandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman iliofanyika nyumbani kwake Maisara Jijini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana akizungumza na kutoa shukrani kwa Wananchi walioitikia wito wa mualiko wa kujumuika katik futari maalum ilioandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj.Othman Masoud Othman nyumbani kwake Maisara Jijini Zanzibar. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman akizungumza na kutowa nasaha zake kwa VIongozi na Wananchi wakati wa hafla ya futari maalum aliyowaandalia katika viwanja vya nyumbani kwake Maisara Jijini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman  akisalimiana na kuagana na Mhe. Nassor Mazrui baada ya kumalizika hafla ya futari maalum aliyoiandaa kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman akisalimiana na kuagana na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyowaandalia Wananchi katika viwanja vya nyumbani wake Maisara Jijini Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, leo amejumuika na viongozi na wananchi wenzake katika futari ya pamoja nyumbani kwake, Maisara, mjini Zanzibar. 

Futari hiyo ilimkutanisha Makamu huyo wa Kwanza wa Rais na viongozi kadhaa wa kiserikali, kidini, vyama vya siasa pamoja na waumini wengine wa wa dini ya Kiislamu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuftari, Alhaj Othman amewataka wageni wake na Wazanzibari kwa ujumla kudumisha amani na umoja uliopo sasa visiwani Zanzibar, ambao ni matokeo ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Aidha amewakumbusha viongozi wenzake wa ngazi mbalimbali kuwajali na kuwathamini raia, kwani wao ndio chanzo cha wao kushika nafasi walizonazo.

"Mkulima mzuri huyajali mazao yake na kiongozi mzuri ni mwenye kuwajali raia wake. Tuwathamini na tuwaunganishe raia wetu waishi kwa umoja na mshikamano", alisisitiza Alhaj Othman

Kwa niaba ya wageni wenzake, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mheshimiwa Idrisa Kitwana Mustafa, amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kwamba watafuata nyayo zao viongozi wakuu kwa kuhamasisha umoja na mshikamano sambamba na kushirikiana katika mambo mbalimbali. 

Futari ya leo ilikuwa muendelezo wa juhudi za Makamu wa Kwanza wa Rais kukutana na wananchi na viongozi na kuwaleta pamoja kwenye azma ya kuyaimarisha na kuyapa nguvu Maridhiano ya Wazanzibari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.