Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Akiondoka Nchini Zanzibar Akielekea Nchini Msumbiji Kuhudhuria Mkutano wa Sadc Unaofanyika leo Jijini Maputo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, 26/5/2021,akielekea Nchini Msumbuji kuhudhuria Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Jijini Maputo Msumbiji.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Msumbiji kuhudhuria Mkoato wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho Jijini Maputo Msumbiji
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,wakati akielekea Nchini Msumbuji kuhudhuria Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho Jijini Maputo
 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Maputo nchini Msumbiji kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika nchini humo Mei 27,2021.

Akiondoka katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Karume Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi aliagwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdallah pamoja na viongozi wengine.

Mkutano huo wa nchi za (SADC) unaofanyika nchini Msumbuji unatarajia kujadili masuala ya hali ya ulinzi na usalama unawajumuisha viongozi wakuu kutoka nchi za Jumuiya (SADC) zikiwemo Msumbiji, Malawi, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini,  na Zimbwabwe.

Rais Dk. Mwinyi anatarajia kurejea nchini Alkhamis ya Mei 27 mwaka huu.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.