Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amezungumza na Mwakilishi
mkaazi wa ‘UN Women Tanzania’ Hodan
Addou, aliefika Ikulu Jijini Zanzibar.
Dk. Mwinyi amesema Serikali iko makini kuhakikisha wanawake wa Zanzibar wanapata haki zao pamoja na kuondokana na vitendo vyote vya ukandamizaji, ikiwemo udhalilishaji dhidi yao na watoto.
Aidha, alisema Serikali imekuwa ikiwateua wanawake zaidi katika nafasi mbali mbali za uongozi sio kwa upendeleo, bali kutokana na juhudi, uwezo na uaminifu mkubwa walionao.
Nae, Mwakilishi Mkaazi wa ‘UN Women Tanzania’ Hodan Addou alitoa pongezi kwa Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi zake za kuimarisha Uwakilishi wa wanawake katika Uongozi, sambamba na juhudi zinazofanyika katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.
Alisema UN Women Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha wanawake wa Zanzibar wanapiga hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi.
Alisema ana imani kubwa kuwa sekta ya Uchumi wa Buluu italeta faida kubwa kwa wanawake, hivyo akaunga mkono juhudi za Serikali zinazoendelea kuchukuliwa kuimarisha sekta hiyo, ili kuinua hali zao kiuchumi.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024
2231822
E-mail: abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment