Habari za Punde

UNGUJA MABINGWA MCHEZO WA KURUSHA TUFE UMISSETA 2021

Na.John Mapepele -Mtwara.

Timu za Unguja na Shinyanga wameongoza kwenye mchezo wa kurusha tufe kwenye mashindano ya Taaluma na Michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye fainali ziolizofanyika leo Juni 26, 2021 mjini Mtwara.

Msemaji wa UMISSETA 2021, Ndg.John Mapepele amesema Abdala Salum kutoka Unguja ameibuka kuwa mshindi wa kwanza baada ya kurusha umbali wa mita 14 na sentimita 30 akifuatiwa na Edward Michaeli kutoka mkoa wa Dar es Salaam aliyerusha umbali wa mita 11 na sentimita 97 wakati nafasi ya tatu imechukuliwa na Rajabu Mtonyi kutoka Mkoa wa Dodoma aliyerusha umbali wa mita 11 na sentimita 47.

Kwa upande wa wasichana Keflonia Daudi kutoka Mkoa wa shinyanga ndiye Msindi wa kwanza kwa kurusha mita 8 na sentimita 93 akifuatiwa na Martha Matinga kutoka Simiyu aliyerusha umbali wa mita 8 na sentimita 88 ambapo nafasi ya   tatu ilichukuliwa na Fatma Saidi kutoka Unguja aliyerusha umbali wa mita 8 na sentimita 70.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.