Habari za Punde

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mhandisi Masauni Atembelea Benki ya TPB na Soko la TMX

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akikabidhiwa kitabu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, alipotembelea Benki hiyo katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akiongoza kikao cha viongozi wa tasisi ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), alipotembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akiongoza mkutano wa Menejimenti ya Benki ya TPB, katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, akieleza hatua mbalimbali ambazo Benki hiyo imechukua katika kuhakikisha inaimarika, wakati wa mkutano wa Menejimenti ya Benki hiyo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Bw. Henry Bwogi, akieleza namna Benki hiyo ilivyojidhatiti kutoa mikopo kwa wanachama wake katika kutekeleza adhima ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, wakati wa ziara Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi (katikati), akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), baadhi ya viongozi waliopita wa Benki hiyo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Picha ya namna Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) linavyofanya kazi.

(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.