Habari za Punde

Wanufaika mradi wa Viungo waanza na lishe bora

Baadhi ya akinana mama wa shehia ya Kivunge mkoa wa kaskazini Unguja wakivuna mboga mboga walizopanda baada ya kupatiwa mafunzo kupitia mradi wa Viungo uliofadhiliwa na umoja wa Ulaya.
Afisa  lishe kupitia mradi wa Viungo mwenye fulana nyeupe akitoa mfunzo kwa akinamama wa Kivunge namna bora ya kuandaa mboga kabla ya kupika ili isipoteze virutubisho.

 Mkulima wa mboga mboga kutoka shehia ya kivunge Mosi Juma akipika mboga baada ya mafunzo ya uandaaji wa mboga yenye virutubisho.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ


Tatizo la ukosefu wa mlo wenye virutubisho kwa akinamama visiwani Zanzibar limeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya wanufaika wa mradi wa viungo kuanza kuvuna mboga mboga na kutumia kama sehemu ya mlo wao wa kila siku jambo ambalo awali hawakua wakilifanya.

 

Hali hio imekuja kufuatia kuanza kwa mavuno ya mboga mboga zenye kurutubisha lishe ambazo wanufaika wa mradi huo awali walipatiwa mafunzo ya kilimo bora na umuhiomu wa kutumia mazao yao kama sehemu ya lishe.

 

Miongoni mwa wanufaika hao kutoka shehia Kheri Khamis Ame mkaazi wa shehia ya Kivunge mkoa wa kaskazini Unguja alisema awali kabla ya mradi huo kuanza hawakua na utaratibu wa kula kile wanachokilima na waliamini wanapaswa kuuza pekee.

 

Alisema licha ya kuwa mazao yao hayakua yakifanya vizuri kutokana na kukosa uweledi wa njia bora za kilimo lakini hawakuweza kutumia mboga hizo kama sehemu ya chakula chao badala yake waliuza na kupata fedha tu.

 

Alieleza kuwa mara baada ya kupata mafunzo walifahamu umuhimu wa kula mboga majumbani na yeye kama baba wa familia hivi sasa ameanza utaratibu maalumu wa kuhakikisha kinacholimwa na kuvuna kinakwenda nyumbani kwanza kabla ya kwenda sokoni kwa ajili ya mauzo.

 

”Ni mra mbili nakumbuka mke wangu alijifungua hospitali na mara zote alitiwa damu baada ya kujifungua nina imani chanagamoto hile sasa itamalizika kwa mke wangu kwani amekua mlaji mzuri wa mboga mboga baada ya kupatiwa mafunzo haya”aliongezea.

 

Nae Mosi Juma Ali wa Kivunge alisema kilimo cha mboga mboga kina faida kubwa sana kwao na kwamba walichokikosa awali ni uatalamu tu na namna bora ya kuzitumia mboga hizo.

 

Alisema baada ya kupata mafunzo akinamama wengi wamehamasika na kilimo cha mboga mboga na kwamba itapunguza chanagamoto waliokua wakikabiliana nayo akinamama wengi hususani wakati wa kujifungua.

 

Sambamba na hayo alisema mauzo ya kilimo hicho pia yatawafanya waweze kuweka hakiba kama kikundi pia mtu mmoja mmoja na kisha kusaidia huduma za kifamilia.

 

Kwa upande wake Afisa lishe na uhakika wa chakula kupitia mradi huo Witness Sima William alisema kuna umuhimu mkubwa wakila binadamu kula mboga mboga ikiwezekana hata kila siku.

 

Alisema mboga ni chakula muhimu kwa binadamu na kinasaidia mfumo mzima wa urutubishaji mwilini pamoja na mmengenyo wa chakula jambo ambalo ni muhimu kwa maisha ya kila siku.

 

Akifafanua zaidi alisema kuna mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uandaaji wa mboga na kwamba unatakiwa kuhakikisha huoshi mboga hio na kupitiliza kwani kufanya hivyo kunaondosha virutubisho muhimu ambavyo vingepaswa kuwemo.


Mradi wa Viungo unatekelezwa visiwani hapa ukilenga kuwanufaisha zaidi ya wanufaika 57,000 kutoka maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba ukitekelezwa na TAMWA-ZNZ,PDF,pamoja na CFP chini ya ufhadhili wa umoja wa Ulaya.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.