RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka watendaji wa Serikali kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma pamoja na misaada ili kuhakikisha matatizo yanayowakabili Wawekezaji yanapungua.
Dk. Mwinyi ametoa wito huo leo katika ufunguzi wa Hoteli ya kitalii ya Nyota tano ya ‘Zanzibar Golden Tulip Airport Hotel’ iliopo pembezoni mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, jijini Zanzibar.
Amesema Serikali imekuja na Sera ya Kuvutia Wawekezaji, hivyo mtendaji yeyote atakaekwenda kinyume au kukwamisha azma hiyo atalazimika kuwa nje ya Serikali.
Alisema hatua ya serikali ya kuleta mabadiliko kiutendaji katika kipindi kifupi kijacho, inalenga kuvutia wawekezaji , na kubaiinisha kuwa wawekezaji wanahitaji utendaji wa kisasa.
Aidha, Dk. Mwinyi amesema tayari Serikali imeanza kuchukua hatua, husuan kwa tasisi zinazotoa huduma kwa wananchi , pamoja na kuhakikisha utendaji katika sekta binafsi unahamia Serikalini.
Rais Dk. Mwinyi alisema serikali ya awamu ya nane kwa kushirikiana na sekta binafsi inakuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya Uwekezaji, hivyo akatumia fursa hiyo kuwahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujitokeza bila khofu kushirikiana an Serikalii katika kupanga na kutekeleza miradi kwa njia ya PPP.
“Utaratibu huu umekuwa ukitumika sasa na kupendwa na wawekezaji katika nchi mbali mbali kw anjia ya Public Private Partneship – PPP”, alisema.
Alisema ujenzi wa Hoteli hiyo unakwenda sambamba na dhamira ya serikali ya kuimarisha sekta ya Utalii, usafirishaji pamoja na biashara.
Alisema kwa kipindi kirefu wasafiri wengi wanaotaka kusafiri nyakati za asubuhi wamekuwa wkaisumbuka kupata malazi ya uhakika karibu na kwianja cha ndege kama ilivyo katika viwanja vyengine vya Kimataifa.
Alisema hoteli hiyo hivi sas aitaqweza kutoa huduma hizo, ikiwa na miumbombinu muhimu na ya kisasa itakayowawezesha kupata huduma muhimju zinazotolewa na mashirika ya Ndege hapa nchini na hivyo kuongeza idadi ya wageni.
Aidha, Dk. Mwinyi alionyesha kufarijika kwake na kusema mbali ya kuwepo changamoto mbali katika sekta ya utalii zinazotokana na kuzuka kwa maradhi ya Corona Covid - 19, bado wawekezaji wa sekta hizo kwa kushiirikiana na Serikali wameendelea kuwekeza mitaji mikubwa hapa nchini.
Katika hatua nyengine Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa Kamapuni ya Estim Construction kwa umakini na umahiri mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo, ambapo pamoja na mambo mbali mbali lina kumbi kubwa za kupendeza kwa ajili ya mikutano ya Kitaifa na Kimataifa.
Mapema, Waziri wa Nchi, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga alisema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa kuimarisha sheria hatua aliyobainisha inalengo la kufungua milango ya Uwekezaji ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa kituo muhimu cha Uwekezaji katika Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Sharif Ali Sharif alisema Mradi wa ujenzi wa Hoteli ya kisasa ulithibitishwa na Mamlaka hiyo (ZIPA) ukiwa na mtaji wa makisio wa Dola za Kimarekani milioni 7.
Alisema kuwa mradi huu ambao utafanya biashara zake kwa jina
la Golden Tulip Inn Airport Hotel, mpaka sasa umeshawekeza zaidi ya Dola za Kimarekani
milioni 9, ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 28 ya makisio ya mtaji wa awali ambapo
hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umeshafikia zaidi ya wastani wa asilimia 90.
Aliongeza kuwa Kampuni ya Royal Group of Companies
tayari imewekeza miradi sita kupitia ZIPA katika sekta ya ukarimu, huduma za uwanja
wa ndege, huduma za biashara na viwanda ambazo zinatoa mchango mkubwa katika maendeleo
ya uwekezaji nchini, kukuza uchumi na kutengeneza ajira hususan kwa vijana.
Sharif alisema kuwa mradi huo umeingiza dhana mpya ya utalii
ijulikanayo kwa jina la “MICE” yenye maana ya Utalii wa Mikutano, Vivutio,
Mikutano ya Kimataifa na Maonyesho ambapo dhana hiyo itasaidia sana kupanua wigo
wa sekta ya utalii na kuacha kutegemea pekee utalii wa hoteli za fukwe.
Akieleza hali ya uwekezaji kwa ujumla kupitia Mamlaka hiyo,
Sharif alisema kuwa tangu kuanza kazi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu
ya Nane mwezi Novemba 2020 hadi kufikia Julai 2021, Mamlaka imefanikiwa kusajili
jumla ya miradi 50 yenye jumla ya mitaji ya Dola za Kimarekeni milioni 321.
Alisema kuwa hali hiyo inaonyesha kuwepo kwa mwamko mkubwa
wa wawekezaji wanaokuja kuwekeza Zanzibar kutokana na Mikakati ya Rais Dk. Mwinyi ya kuimarisha na
kuvutia uwekezaji nchini.
Mapema,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya “Royal Group of
Companies” Hassan Mohammed Raza alisema kuwa jengo hilo liliwekewa jiwe la
msingi Januari 4, 2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaaliwa baada ya ujenzi kuanza rasmi mnamo Februari mwaka 2019.
Alisema kuwa Hoteli hiyo itakuwa na hadhi ya Nyota tano yenye
vyumba 60 ambapo lengo na madhumuni ya ujenzi huo karibu na uwanja wa ndege utasaidia
malazi karibu na uwanja wa ndege hususan kwa wasafiri wa ndege za usiku sana au
alfajiri, wafanyakazi wa ndege na abiria ambao ndege zao zinachelewa kuruka au
safari zilizofutwa.
Alisema kuwa hoteli hiyo itakuwa na kumbi tatu za mikutano
wenye uwezo wa kuchukua watu 40, 200 na mwengine utakuwa na uwezo wa kuchukua watu
1,000 ambapo pia, itakuwa na mikahawa, bwawa la wazi la kuogelea na sehemu ya kucheza
watoto.
Alisema kuwa jumla ya Dola za Kimarekanimilioni
9 zimewekezwa hadi kukamilika ujenzi wa hoteli na ukumbi mkubwa wa mikutano ambapo
matarajio ni kuendelea na uwekezaji zaidi na kufikia katiya Dola milioni 13
hadi 15.
Aidha, alingeza kuwa hoteli hiyo imejengwawa kuzingatia masharti
na ubora unaohitajika kwa hoteli ya uwanja wa ndege ambapo miongoni mwao ni pamoja
na vioo vya madirisha vya kuzuia kelele za ndege.
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail: abdya062@gmail.com.
No comments:
Post a Comment