Habari za Punde

KANDA YA SMZ YASHINDWA KUTETE UBINGWA WAKE WA JUMLA KATIKA MICHEZO YA MAJESHI TANZANIA BAMMATA NA KUAMBIA USHINDI WA TATU

Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene akimkabidhi Kombe kepten wa timu ya Kanda ya SMZ Mwinjuma Mwinyi Majio baada ya kumaliza mchezo kwa sare ya goli 1kwa 1 na kuamuliwa kwa mikwaju ya penanti ya magoli 4 kwa 5.
Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene akipokea heshima ya Gwaride la wanamichezo wa Michezo ya Majeshi (BAMMATA aliyoyafunga jana Agosti 13 katika Kiwanja cha Jamhuri Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene akikagua kikosi cha Timu ya mpira wa miguu cha Kanda ya SMZ iliyocheza fainali na timu ya kanda ya Polisi katika kiwanja cha Jamhuri Dodoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Meja Jenerali Amri Salim Mwami akitoa salamu za Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi CDF Jenerali Venance Mabeo katika sherehe ya kufunga Michezo ya Majeshi Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene akizungumza na wanamichezo wa Kanda saba zilizoshiriki Michezo ya Majeshi Tanzania BAMMATA katika hafla ya kufunga michezo hiyo iliyofanyika Kiwanja cha Jamhuri Dodoma.

Picha kikosi na benchi la ufundi la Timu ya mpira wa miguu ya Kanda ya SMZ wakiwa na kombe lao walilolitetea walilokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene.

Picha na Makame Mshenga KMKM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.