Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na Mabalozi wa nchi za Kuwait, Ujerumani na Rwanda Ikulu leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania. Mhe.Mubarak Mohammed Alsehaijan, alipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Kasha mgeni wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe.Mubarak Mohammed Alsehaijan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,25/8/2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Mhe.Maj.Gen.Charles Karamba, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, leo 25/8/2021.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regina Hess, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazunguzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo na Ushirikiano Ubalozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Dr.Katrin Bornemann, wakati wa mazungumzo na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe. Regina Hess. (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 25, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.

 Mhe. Rais awali alikutana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mubarak Mohammed Alsehaijan.

 
Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuendeleza uhusiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar pamoja na kuipatia Zanzibar misaada mbalimbali katika sekta za kijamii.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Dk. Mwinyi alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda, Meja Jenerali Charles Karamba. Katika mazungumzo hayo Balozi Karamba alimueleza Mhe Rais mpango wa Shirika la Ndege la Rwanda ‘Air Rwanda’ kuanza safari zake kati ya Kigali na Zanzibar ifikiapo katikati ya mwaka 2022, hatua ambayo itaimarisha sekta ya utalii kwa Zanzibar na Rwanda.
 
Balozi Karamba alitumia nafasi hiyo pia kumtaarifu Mhe. Rais juu ya mwaliko maalum waliouleta Zanzibar wa kuanzisha Ushirikiano baina ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB) unaolenga ushirikiano wa kiuwekezaji na kuwa na kituo kimoja cha kibiashara baina ya Zanzibar na Rwanda.
 
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Regina Hess ambaye alifika Ikulu Zanzibar kuelezea mipango ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Zanzibar na Ujerumani hususani kwenye eneo la uboreshaji wa huduma za maji na michezo.

Mapema, Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alikutana na Mwakilishi wa Heshima wa Jamhuri ya Slovakia nchini Tanzania Bwana Moustafa  Khataw ambaye alimtaarifu Mhe. Rais mpango wa kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Slovakia mpaka Zanzibar.

Kwa upande wake Rais Dk. Mwinyi alimtaka Mwakilishi huyo kushajiisha wawekezaji wa Slovakia na kusisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatilia mkazo dira ya Uchumi wa Buluu, ikiwemo uvuvi wa bahari kuu pamoja na Mafuta na Gesi huku akibainisha kuwepo rasilimali za kutosha baharini ambazo bado hazijatumika ipasavyo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.