Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekabidhi Vifaa Vya Afya na Gari la Wagonjwa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba .

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga moto  gari la Wagonjwa kabla ya kulikabidhi kwa Uongozi wa Hospitali  ya  Abdalla Mzee Mkoani Pemba lililotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani  Pemba Mhe.Abdalla Hussein Kombo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo ilioko katika Wilaya ya Mkoani Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi ufunguo wa gari la wagonjwa Daktari Mkuu wa Mkoa (OMD) ambae pia ni Mkurugenzi Baraza la Mji Mkoani Dkt.Mohammed Faki Said ,kwa ajili ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, lililotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Pemba Mhe.Abdalla Hussein Kombo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo Mkoani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akikabidhiwa Mashine ya Kungolea Meno na Vifaa mbalimbali vya Afya  kwa ajili ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba na Mfanyabiashara Maarufu wa  Zanzibar Bw.Said Nassir Nassor (Bopar) hafla hiyo imefanyika katika  ukumbi wa Hospitali hiyo Mkoani Pemba 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa  na galoni  la vitakasa mikono  baada ya kukabidiwa na Mfaanyabiashara maarufu  wa Zanzibar Bw.Said Nassir Nassor, na kukabidhi kwa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo imefanyika katika Hospitali hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba Dkt..Haji Mwita akitowa maelezo wakati akitembelea chumba cha X-Ray katika hospitali hiyo akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi Vifaa mbalimbali vya Afya na Gari ya Wagonjwa  kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo, wakati  ziara yake  katika Mkoa wa Kusini Pemba
WAUGUZI wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na  Uongozi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba
WANANCHI wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya kumaliza kukabidhi vifaa mbambali vya Afya na Gari ya Wagonjwa.hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.