Habari za Punde

SERIKALI KUFIKISHA HUDUMA YA INTANETI, SIMU NYUMBA ZA TEMBE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka wakisaini mkataba wa ushirikiano baina ya Wizara hiyo na TANESCO ya ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme, Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma wa kwanza katikati ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na kulia kwake ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Dkt. Tito Mwinuka wakibadilisha mkataba wa ushirikiano baina ya Wizara hiyo na TANESCO ya ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme baada ya kusaini, Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile, kulia kwake ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza baada ya kushuhudia zoezi la utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara hiyo na TANESCO kukamilika wa ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme uliofanyika Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza baada ya kushuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na TANESCO kukamilika uliofanyika Dar es Salaam. Aliyeketi chini ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza mbele ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. (hawapo pichani) kabla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na TANESCO kukamilika uliofanyika Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso akizungumza baada ya kushuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na TANESCO wa ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme uliofanyika Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali akitambulisha Viongozi wa Wizara ya Nishati katika halfa ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na TANESCO wa ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme uliofanyika Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anne Kilango Malecela baada ya kushuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na TANESCO wa ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme uliofanyika Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akizungumza kabala ya hafla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na TANESCO wa ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme uliofanyika Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.