Habari za Punde

Wanawake wana uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu - Dk Mzuri Issa

Mwandishi wa habari kutoka Tumbatu FM Makame Pandu Makamae (katikati) akieleza mfano wa kisia ambacho alikifanyia kazi na kuleta matokeo chanya kupitia redio Tumbatu.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali Zanzibar wakifuatilia mafunzo ya siku tatu yaliotolewa na TAMWA-ZNZ kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

 Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akizungumza kuhusu umuhimu wa wanawahabari kujikita na kupaza sauti za wanawake ili waweze kushiriki katika nafasi za uongozi na demokrasia.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

 

Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema ushiriki wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi wa kisiasa na kijamii huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii za na Nchi kwa ujumla, kwani wanawake ni watu weye uwezo mkubwa na wepesi wa kutekeleza majukumu yao.

 

Dkt,Mzuri aliyasema hayo wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku 3 ya waandishi wa habari 30 wa vyombo mbali mbali Zanzibar kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia.

 

Alieleza kuwa Taifa lolote lile  haliwezi kupiga hatua za kimaendeleo zaidi iwapo litawaacha wanawake nyuma na kuendeleza imani yakuwa  wanawake hawapaswi kuwa viongozi katika nyanja za kitaifa na hata kijamii.


Alisema licha ya   harakati mbali mbali zinazoendelea kufanyika visiwani Zanzibar kuhakikisha idadi kubwa ya wanawake wanashiriki kwenye uongozi bado hadi sasa hali hio haijaridhisha na wapo baadhi ya wenye nyadhifa au kuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii wanaamini mwanamke hapoaswi kuwa kiongozi jambo ambalo si uhalisia.


Aidha Mkurugenzi huyo alifafanua na kwenda mbali zaidi kwa kueleza wapo baadhi ya watu kwa kutokuelewa wamekau wakitumia vipengele vya imani za dini kukandamiza wanawake wanapotaka kugombea kwenye uongozi licha ya kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwa viongozi na mitazamo hio ya dini haijamkataza mwanamke kuwa kiongozi.

 

Katika hatua nyengine alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya wanajamii kuendelea kuamini kuwa kushiriki kwa wanawake kwenye uongozi ni chanzo kikubwa cha uhuni huku wakisahau pia uhuni huo unaweza kufanywa hata na wanaume wanapokua kiongozi lakini kwa makusudi ya kuwachafua wanawake jamii imebeba taaswira hio potofu.


Awali mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo umelenga kuwafikisha wanawake elfu sita kutoka wilaya kumi na moja za Unguja na Pemba.


Alisema wanufaika wote wa mradi huo watajengewa uwezo dhidi ya ushiriki wa wanawake katika uongozi na umuhimu wa demokrasia.


Mradi huo wa miaka mine unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na ZAFELA pamoja na PEGAO chini ya ufhadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.