Habari za Punde

Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Tiba ya Mazoezi ya Viungo.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Nassor Ahmed Mazrui  akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wakufunzi wa PhysiotheraPY  kuhusu huduma ya Matibabu ya Viungo kwa njia ya mazoezi ikiwa ni siku ya maazimisho ya kila  mwaka wanafisiotherapia yanayoadhimishwa Duniani kote.


Na Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema kada ya utoaji huduma ya afya kwa njia ya mazoezi ya viungo (Physiotherapy) ni muhimu kwa ajili ya matibabu kwa jamii.

Waziri Mazrui ameyasema hayo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA huko Vuga wakati wa kuadhimisha Siku ya Fisiotherapia, amesema wanafisiotherapia wana uwezo mkubwa wa kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya viungo kupata huduma bora na kuimarisha  afya kwa jamii.

Amesema kuwa kada hiyo ni adhimu nchini  ni vyema jamii ipate elimu na  uwelewa mzuri  wa kupata matibabu kwa njia ya mazoezi ili  kuiinua zaidi  kitaaluma na kuweza kuthaminiwa.

Amewasisitiza wanafunzi wa kada ya fisiotherapia kuchangamkia fursa ili kuimarisha fani hiyo na kuinuka kitaaluma kwa lengo la kutoa huduma kwa ufanisi na umahiri mkubwa na kuitangaza.

Waziri Mazrui ameahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto zinaikabili kada hiyo kwa kushrikiana na uongozi wa Chuo kwa kuwatia walimu pamoja na vifaa ili kuondosha tatiz hilo chuono hapo.  

Mapema Mkuu wa Skuli ya Afya, Sayansi na Tiba Dk. Ali Said Yussuf ameiomba  serikali kuwapatiwa walimu wa kudumu kwa lengo kutoa taaluma bora na kupata wahitimu mahiri wenye ujuzi.

Ameleza kuwa  kada ya fisiotherapia inatoa huduma huduma za mazoezi ya viungo kwa wagonjwa wenye maradhi mbalimbali ikiwemo shindikizo la damu, saratani, uti wa mgongo, uviko 19, watoto wenye usonji, mtindio wa ubngo pamoja na  vichwa maji ili kuimarisha afya za wagonjwa hao.

“Matibabu ya kada hii yanasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa na wasiokuwa wagonjwa kwasababu kuna baadhi ya watu wanapata matatizo mbalimbali ya viungo kutkana na kukaa muda mrefu pamoja na kuumia katika michezo”, alieleza Mkuu huyo.   

Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya, Sayansi na Tiba Profesa Amina Abdulkadir amesema matibabu ya Fisiotherapia hufanywa kwa kuondoa matatizo ya  viungo yanayoonekana nayasiyooneka ili kuimarisha afya kwa jamii.

Nao wanafunzi wa kada hiyo ya fisiotherapia wameomba kupatia chanjo ya ugonjwa Ini kwani wanafanyakazi katika mazingira hatarishi pale wanaofanya mafunzo ya vitendo,  kupatiwa mafunzo ya ujasiri amali ili watapomaliza kuweza kujiajiri pamoja na kuwekewa kituo katika chuo kitakachorahisihsa kutoa mafunzo ya vitendo chuoni hapo.

Siku ya Physiotheapy duniani huadhimisha kila ifikapo tarehe 08 Septemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.