Habari za Punde

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman : Awaomba Wananchi wa Jimbo la Konde Pemba Kumchagua Ndg.Mbarouk Amour Habib, Katika Uchaguzi Mdogo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe Hemed Suleiman Abdulla akimnadi na kumuombea Kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Konde Pemba Ndg. Mbarouk Amour Habib, katika mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika katika viwanja vya Makangale Pemba, katika mkutano wa ufungaji wa kampeni.



Mjumbe wa kamati ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayotekeleza ilani ya CCM imepanga kuzikarabati na kuzijenga barabara zote za ndani kwa kiwango cha lami zikiwemo barabara zinazopatikana ndani ya jimbo la Konde.

Mjumbe huyo wa kamati kuu ameleza hayo wakati akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Konde kupitia mkutano wa ufungaji wa kampeni wa jimbo hilo uliofanyika katika uwaja wa Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema serikali kupitia ilani ya uchaguzi ya 2020-2025 itaimarisha maendeleo kwa kuwanufaisha wananchi wa jimbom la konde na Zanzibar kwa ujumla.

Mhe. Hemed alifafanua kuwa, miongoni mwa barabara zitakazaojengwa kupitia mradi huo ni pamoja na barabara ya konde, Msuka hadi Makangale.

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais amesema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi imejipanga kufikisha huduma ya nishati ya umeme katika maeneo yote ambapo hadi sasa serikali inaendelea na maandalizi ya kupunguza gharama za ungaaji wa umeme ili kuwarahishia wananchi wake juu ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Ameleza kuwa,zoezi la ufikishaji wa nguzo katika makaazi ya watu litagharamiwa na serikali ambapo mwananchi hatatozwa gharama yoyote kwa ajili ya ununuzi wa nguzo hizo.

Akimuombea Kura mgombea huyo kwa tiketi ya CCM Mhe. Hemed amesema Chama cha Mapinduzi kinamuuamini Ndugu Mbarouk kutokana uwezo na sifa alizonazo katika kuwatumikia wananchi.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa amesema Chama cha Mapinduzi kimejipanga katika uchaguzi huo na kina Imani na mgombea kutokana na kapeni za kistarabu alizoziendesha katika jimbo hilo kwa kuwafikia wapiga kura wengi ndani ya jimbo hilo.

Kwa upande wake Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Konde kupitia CCM Ndugu Mbarouk Amour Habib amewaahidi wananchi wa Jimbo hilo kuwa pindipo akipata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo kwa kushirikiana na viongozi wenzake atahakikisha wanakarabati madarasa yote ya skuli ya msingi Makangale ili kuweka miundombinu mizuri ya kusomea wanafunzi.  

Mapema asubuhi Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM taifa amekagua ujenzi wa Ofisi za chama za CCM  Mkoa wa Kusini Pemba zilipo Chachani wilaya ya Chakechake.

Akikagua Jengo hilo Mhe. Hemed ameridhishwa na maendeleo mazuri ya ujenzi na kueleza kuwa imefika wakati Ofisi za chama cha Mapinduzi ziendane na hadhi ya chama kinachoongoza dola ili kutoa faraja kwa watendaji wake kufanya kazi katika mazingira yanayoridhisha.

Pia Mhe. Hemed amekagua ujenzi wa jengo la kitega uchumi linalogharamiwa na CCM Mkoa wa Kusini Pemba na amesema kukamilika kwa jengo hilo kutatoa fursa mbali mbali kwa vijana katika kujiajiri.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Oktoba 06, 2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.