Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi awakaribisha wawekezaji kuwekeza Tanzania

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amewaalika wawekezaji kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nyingine duniani kuja kuwekeza Zanzibar na Tanzania Bara.


Alisema hayo wakati akifunga Onesho la Kwanza la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoanza Oktoba 9, mwaka huu na kuhitimishwa jana jijini Arusha.

Aidha, alisema kuwa katika visiwa vya Zanzibar kuna maeneo mengi ya uwekezaji hususan katika uchumiwa Buluu kupitia bahari na maeneo mengine kama ya utalii wa kitamaduni.

Rais Dk Mwinyi alisema kuwa nchi za EAC zina vivutio vilivyopi karibu kila eneo, hivyo nchi hizi zifanye jitihada kuwavutia watalii wengi wengi zaidi ili vivutio hivyo vichangie zaidi katika maendeleo ya nchi hizo.

Alisema katika nchi za EAC, pia kuna vivutio vingi vilivyopo karibu kila eneo, hivyo nchi hizo zifanye jitihada kuwavutia watalii wengi zaidi ili vivutio hivyo vichangie zaidi katika maendeleo ya nchi hizo.

“Ripoti ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) inaonesha kwamba idadi ya watalii wanaokuja ni asilimia 8.6 ya watalii wote wanaokuja Bara la Afrika wakati idadi hiyo ni sawa na asilimia 0.3 ya watalii wote duniani,” alisema Dk Mwinyi.

Alisisitiza kwamba iIdadi hiyo ni ndogo kulingana na watalii wanaokuja Afrika hivyo jitihada zaidizinahitajika ili kuongeza idadi ya watalii zaidi.

Alisisitiza jitahada zaidi kufanyika ili kuongeza idadi ya watalii hasa baada ya janga laCovid-19 kujitokeza na kwamba licha ya janga lazima utalii na vivutio vyake utangazwe ili kuhakikisha watalii wengi zaidi wanakuja katika nchi za EAC ikiwamo Tanzania.

Alisema kwa sasa mapato yanayotokana na utalii hayaendani na wingi na ubora wa vivutio vya utalii vilivyopo na akasema nchi za EAC ikiwamo Tanzania zina utajiri wa vivutio vya utalii vikiwamo hasa vya asili.

Alizihimiza nchi za EAC kuboresha sera za utalii ili kusaidia wawekezaji katika sekta yautalii kufanya kazi kwa ufanisi.

Alisema serikali inasisitizia uchumi wa bluu kwani zipo fursa za kuwekeza katikahoteli, meli za kitalii, michezo ya bahari na masuala mengine ya utalii na uchumi.

Alisema Zanzibar imefungua fursa nyingi za uwekezaji ukiwemo uvuvi katika bahari kuu,majengo, utafutaji wa mafuta na gesi na kusisitiza kuwa, Zanzibar ni njema na anayetaka aje.

Katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro alisisitiza kuwa,sekta ya utalii katika EAC, imeleta sura mpya kwa nchi hizo katika masuala yautalii.

Alisema onesho kama hilo litafanyika mwakani nchini Burundi na kuwa baada ya onesho hilo kumalizika jana, waoneshaji watapata fursa za kwenda kutembelea vivutio vya utalii vya hifadhi za taifa za Mkomazi, Serengeti, Mlima Kilimanjaro,Ngorongoro na vivutio vingine vya utalii vilivyopo Zanzibar.

DkNdumbaro alisema onesho hilo limewashirikisha waoneshaji wakubwa wa bidhaa za utalii zaidi ya 100 huku waoneshaji 41 wakitoka katika nchi 19 za Afrika, Ulayana Marekani. Nchi zote sita wanachama wa EAC zilishiriki na hivyo kufanya jumla ya nchi 25 zilizoshiriki.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara wa EAC, Kenneth Bagamuhunda kwa upande wake alisema kuwa maonesho hayoyalipaswa kuanza mapema, hivyo kwa mwanzo huo mzuri unaonesha mwamko wakuungana pamoja kwa nchi za EAC katika kutangaza utalii kwa kila nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.