Habari za Punde

Matukio ya Picha Kisiwani Pemba.

MSAIDIZI Afisa Mradi wa kujenga uelewa kwa vijana katika kuzuia Migogoro ya ukatili kipindi cha mavuno ya zao la Karafuu Pemba Ndg.Omar Abrahman Suleiman, akizungumza na wananchi wa Mgogoni Kifundi Wilaya ya Micheweni, wakati wa Mkutano wa kutoa uelewa juu ya kujenga amani ya Jamii, mradi unaotekelezwa na Jumuiya ya YETA Pemba.
WANANCHI wa shehia ya Mgogoni Kifundi Wilaya ya Micheweni, wakifuatilia kwa makini mkutano wa kutoa uelewa juu ya kujenga amani ya Jamii, kupitia mradi wa kujenga uelewa kwa vijana katika kuzuia Migogoro ya ukatili kipindi cha mavuno ya zao la Karafuu Pemba, mradi unaotekelezwa na Jumuiya ya YETA Pemba

MRATIB wa Jumuiya ya YETA Pemba Zadida Abdallah Rashid, akiorodhesha majina ya wananchi walioshiriki katika mkutano wa kutoa uelewa juu ya kujenga amani ya Jamii, kupitia mradi wa kujenga uelewa kwa vijana katika kuzuia Migogoro ya ukatili kipindi cha mavuno ya zao la Karafuu Pemba, mradi unaotekelezwa na Jumuiya ya YETA Pemba.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.