Habari za Punde

Mhe. Rais Samia akutana na Timu ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na kuwapongeza Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu, kufuatia kufuzu kushiriki katika Kombe la Dunia kwa Watu wenye Ulemavu 2022 Nchini Uturuki. Hafla hiyo iliyoambatana na Chakula cha Mchana imefanyika leo tarehe 07 Disemba 2021 katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu  ambao wamefuzu kushiriki katika Kombe la Dunia kwa Watu wenye Ulemavu 2022 Nchini Uturuki wakiwa katika hafla hiyo katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu baada ya kuzungumza nao leo tarehe 07 Disemba 2021 katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.