Na Mauwa Mohammed Zanzibar
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman amesema ameamua kuomba nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho ili apate nafasi ya kushirikiana na wenzake katika kutimiza malengo ya chama hicho.
Hayo aliyasema mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo huko Afisi Kuu ya Chama Vuga Mjini Zazniabr.
Alisema nafasi itampa uwezo mkubwa wa kutoa mawazo yake ya kukuendesha chama hicho ili lengo kushika dola lifikiwe.
Pia alieleza akipata nafasi hiyo ya chama itamsaidia kurahisisha shuhuli zake za kukijenga chama wakati yuko Serikalini
Alibainisha kuwa nafasi aliyopewa ni kuendesha mambo ya Zanzibar lakini atakuwa na uwezo wa kufanya kazi za siasa Pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sambamba na hilo Mgombea huyo alisema kuwa vyama vya Siasa ndio chem chem ya fikra na kuwataka wanasiasa wasisubiri kuleta hoja wakati wa chaguzi wao ndio waanzishe mijadala mbali mbali ya kuleta mabadiliko.
“Mengi yanayohitaji fikra lazima tuayaazishe kwenye vyama ili tuwe na maendeleo bora ya kiuchumi na kisiasa ikiwemo mabadiliko ya Katiba” alisema Othman
Kwa upande wake mwengine Othman alieleza kuwa Heshima kubwa aliyoipewa katika chama ACT wazalendo kwa kumuamini kupewa nafasi ya Umakamu wa kwanza wa Rais katika Serikali ya mapinduzi Zanzibar ameona na yeye aombe nafasi hiyo ili ashiriki katika kukijenga chama hicho .
“Sasa kuna mambo watu walitegemea nifanye Chama kama alivyokuwa Maalim Seif lakini kumbe sina mamlaka ya kuyafanya haya kwa sababu sina nafasi hiyo kwenye Chama” alisema
Alifahamisha kuwa kuwa nafasi hizo mbili nifursa ya kufanya mambo hayo sehemu nyingi kwa pamoja.
Pia alieleza kuwa atashirikiana na wenzake ili changamoto zote zilizomo kwenye chama chao ili kujenga tasisi imara.
“Chama hichi kinautajiri mkubwa sana ya watu wanaojua na weledi wa siasa kwa kila daraja ambao wako ndani ya chama nje ya chama ambao tukishirikiana kwa pamaoja tunaweza kuleta mabadiliko makubwa” alisema Mgombea huyo.
Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho Muhene Said Rashidi alisema kuwa Mgombea huyo ametimiza vigezo vya kuwa mgombea kwa kuwa mwanachama hai.
Akielezea Mfumo wa Serikali ya Umaoja wa Kitaifa alieleza hautakiwi uwe wa kugawana vyeo unatakiwa kuwa wa kushirikisha mawazo na Majukumu katika kuamua jambo lenye maslahi na nchi.
“Lakini muundo wa JNU haukuwa wa mtoto lalalala bali ni mfumo wa dhati kuwa kuwepo na muendelezo katika nyanja za serikali ili kuimarisha JNU” alisema Othman.
Alibainisha kuwa kuna mifumo mbali mbali ya JNU duniani kila mfumo una msingi yake ambayo imekuwa ikitumika.
“Tukubali mfumo wetu ulianza katika msingi wa matatizo tuliyokuwa nayo na tulipoiunda si kila mtu aliunga mkono lakini tutafika“alisema masoud.
Hata hivyo amebainisha kuwa katika hayo bado yapo mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuweza kuimarisha Serikali ya Umoja wa kitaifa (JNU) ya maendeleo bora zanzibar.
No comments:
Post a Comment